Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Kiwanda cha mionzi tiba nchini kuanza kufanya kazi Juni
Afya

Kiwanda cha mionzi tiba nchini kuanza kufanya kazi Juni

Dk. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Spread the love

 

NAIBU Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, amesema kiwanda cha kutengeneza mionzi inayotibu ugonjwa saratani, kinatarajiwa kuanza kufanya kazi Juni, 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Dk. Mollel ametoa taarifa hiyo leo Jumatatu, tarehe 9 Mei 2022, bungeni jijini Dodoma, akimjibu Mbunge wa Mtambwe, Khalifa Mohamed Issa, aliyetaka kujua Serikali ina mkakati gani wa kuanzisha kiwanda cha kuzalisha mionzi tiba.

Naibu Waziri huyo wa afya, amesema, Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho.

“Kiwanda cha kutengeneza mionzi ya dawa kwa Afrika, nchi nne za Afrika zilikuwa na uwezo wa kuwa kiwanda hiko na sasa Rais Samia amewezesha na tayari kiwanda hicho kipo. Juni kinaanza kazi rasmi,” amesema Dk. Mollel.

Katika hatua nyingine, Issa aliiishauri Serikali ianzishe tume maalumu ya kushughulikia magonjwa yasiyoambukiza, ili kuyadhibiti yasiendelee kuongezeka, ikiwemo saratani na magonjwa ya moyo.

“Magonjwa haya yasiyokuwa ya kuambukiza yanaongezeka kila uchao, mfano kuanzia 2016 tulikuwa na wagonjwa 4,000,000, kufika 2020 wagonjwa wamekuwa 4,800,000 na inagharimu asilimia 20 ya bajeti ya Wizara ya Afya na kusababisha vifo, Serikali hamuoni ni wakati umefika magonjwa haya kuyaundia tume maalumu ya kuyashughulikia ikiwemo saratani,” amesema Issa.

Akijibu swali hilo, Dk. Mollel amesema Serikali itafanyia kazi ushauri wake.

Aidha, Mollel amesema ni bora Serikali ikatumia fedha katika kuyakinga moja kwa moja magonjwa hayo badala ya kuanzisha tume maana fedha zitaishia kwenye masuala ya utawala.

“Tutafanyia upembuzi yakinifu wazo lake, lakini kikubwa ni kuongeza nguvu zaidi kwenye kuelimisha hasa magonjwa yasiyoambukiza, namna mtindo wa maisha na mambo mengine, ili kupunguza watu wanaopata matatizo hayo, lakini kuongeza bajeti kwenye utoaji elimu ili iwafikie wengi,” amesema Dk. Mollel na kuongeza:

“Maana yake ukianzisha taasisi wakati mwingine tunarudi kulekule, fedha nyingi zinaishia kwenye masuala ya utawala badala ya kumfikia mgonjwa mhusika, nafikiri muhimu kuongeza nguvu kwenye eneo hilo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

error: Content is protected !!