December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kiungo Yanga afungiwa miezi 14

Spread the love

KAMATI ya kuzuia na kupambana na dawa zisizo ruhusiwa michezoni ya kanda ya tano Afrika (RADO) imemfungia kiungo wa Yanga, Mohamed Issa ‘Banka’ kujihusisha na mchezo wa soka kwa kipindi cha miezi 14. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Adhabu hiyo ya Banka inaanza kuanzia tarehe  19 Deseemba, 2017 mpaka Febuari 8, 2019 kutokana na matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi. 

Kiungo huyo ambaye alisajiriwa kutoka Mtibwa Sugar katika dirisha kubwa la usajiri alikutwa akitumia dawa hizo katika michuano ya CECAFA Chalenji, iliyofanyika Kenya mwaka jana, baada ya kumchukua vipimo vya mkojo na kwenda kufanyiwa uchunguzi kwenye maabara ya WADA iliyopo Doha, Qatar.

Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo amesema kuwa wakati wote huo Banka hataruhusiwa kufanya chochote kinachohusiana na  michezo ikiwa ni kufanya mazoezi hadharani au kuonekana akishiriki shughuli za mpira wa miguu.

“Baada ya uchunguzi wa maabara na utetezi toka kwa mchezaji huyo, Kamati imemkuta na hatia na imemfungia kwa kipindi cha miezi 14 kuanzia Desemba 9, 2017 na adhabu inatarajiwa kumalizika Februari 8,2019,” alisema Ndimbo.

Hata hivyo baada ya kumkuta na hatia mchezaji huyo alikiri kosa na kuchagua kujitetea kwa njia ya maandishi baada ya kutakiwa kukubali au kukataa kosa na utetezi wake uliwasilishwa 1 Agosti, 2018 juu ya matumizi ya dawa hizo ambazo zinapigwa marufuku michezoni.

error: Content is protected !!