August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kiungo Genk kuchukua nafasi ya Kante Leicester City

Wilfred Ndindi

Spread the love

MABINGWA watetezi wa ligi kuu nchini England, Leicester City wanatarajia kukamilisha usajili wa kiungo Wilfred Ndindi raia wa Nigeria anayekipiga katika klabu ya KRC Genk ya Ubergiji katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari kwa ada ya uhamisho wa pauni 15 milioni kwa mkataba wa miaka mitano.

Kiungo huyo ambaye mpaka sasa amecheza michezo 23 akiwa na klabu yake ya Genk kwa msimu huu na amefunga mabao matatu, anatazamiwa kuwa mbadala wa Ngolo Kante aliyetimkia Chelsea katika usajili wa dirisha kubwa na hivyo nafasi hiyo kukosa mtu wa aina yake.

Usajili wa Ndindi unaweza kuwa wa maana ndani ya kikosi hicho kutokana na aina yake ya uchezaji katika sehemu ya katikati ya uwanja, huku akileta muunganiko ndani ya timu wakati wa kushambulia na huenda akampa unafuu kocha wa kikosi hicho Claudio Ranier ambaye hana mwenendo mzuri kwa sasa kwenye ligi licha ya kupata matokeo mazuri mwisho wa wiki dhidi ya Manchester City.

Mpaka sasa Leicester City imecheza jumla ya michezo 15 ya ligi hiyo ikishinda na kupoteza michezo minne na kwenda sare michezo saba, hivyo kujikusanyia jumla ya alama 16 na kushika nafasi ya 14 katika msimamo wa ligi na hivyo hawana budi kufanya usajili kwa ajili ya kuimalisha kikosi chao kuelekea mzunguko wa pili wa ligi.

Katika muendelezo wa ligi hiyo, Leicester City itakuwa na kibarua leo mbele ya Bournemouth katika uwanja wa King Power huku kiungo wao Danny Drinkwater akitarajia kurejea uwanjani baada ya kutumikia adhabu yake ya kutocheza michezo mitatu.

error: Content is protected !!