January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kituo kikubwa TEHAMA kujengwa Dar

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbarawa

Spread the love

WAZIRI wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa amesema, wizara hiyo inatarajia kujenga kituo kikubwa cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kitakachotumika kuhifadhi taarifa zote za serikali. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Kituo hicho kitajengwa Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambacho kitagharimu Dola za Marekani Millioni 93.77 na kwamba, kituo hicho kitakamilika ifikapo Septemba mwaka huu.

Kituo hicho pia kinatarajiwa kuwa na ubora wa hali ya juu kuliko vituo vyote vya Afrika Mashariki na kuwa, kitakuwa na uwezo wa kuhifadhi taarifa zote hata pindi umeme utakapokuwa umekatika.

Lengo la kituo hicho ni kuweza kukuza Teknolojia ya Mawasiliano nchini, pia wizara ina mpango wa kuhakikisha TEHEMA inafika vijijini.

Prof. Mbarawa amezungumza hayo leo Jijini Dar es Slaam mara baada ya kumaliza kongamano lililoandaliwa na Kampuni ya Huawei kwa kushirikiana na sekta ya TEHAMA (ICT).

Aidha, kongamono hilo ni la siku mbili ambalo linafanyika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, ambapo limewashirikisha wadau mbalimbali wa  ICT wakiwemo wa serikali na sekta binafsi.

Prof. Mbarawa amesema, kongamono hilo lenye maada ya “Rahisisha Teknolojia” lina malengo ya kuzungumzia hali ya sasa ya sekta ya TEHAMA na kujadili namna ya kuiendeleza.

Pia, ndani ya kongamano hilo, Kampuni ya Huawei wamesaini mkataba na TEHAMA ili kuipa nafasi kampuni hiyo kuwa mshauri wa mambo ya TEHAMA nchini. Huawei ni wabunifu wakubwa wa bidhaa za huduma za TEHAMA.

Mtendaji Mkuu wa Huawei Tanzania, Zhang Yongquan amesema, kampuni yao  imekuwa nchini hapa kwa miaka 17 sasa na  imeshiriki katika shughuli nyingi za kiuchumi pamoja na kijamii.

“Tunaishukuru Serikali ya Tanzania pamoja na wizara hii kwa kuendelea kuiunga mkono kampuni yetu,” amesema.

error: Content is protected !!