June 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kituo cha polisi chachomwa moto Dar

Kituo cha Polisi kikiteketea na moto

Spread the love

WANANCHI wamechoma kituo cha Polisi Bunju A, jijini Dar es Salaam, baada ya mwanafunzi (jina halijapatikana) kugogwa na gari na kufariki. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Baada ya kuchoma kituo hicho, walianza kupiga mawe baadhi ya magari yaliyokuwa yakipita katika eneo hilo.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema, wananchi hao waliamua kuchukua maamuzi hayo baada ya polisi kufyatua mabomu ya machozi na risasi za moto kuwatawanya baada ya kufunga barabara kufuatia kifo cha mwanafunzi huyo.

Hata hivyo umma huo uliwazidi polisi nguvu ndipo polisi wakalazimika kukimbia na gari lao huku wakikiacha kituo hicho bila ulinzi hivyo kutoa nafasi kwa wananchi kukichoma bila kizuizi.

Kabla ya kuchoma kituo hicho, waliwatoa mahabusu waliokuwa kizuizini ndani ya jengo la kituo.

Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura ili kuzungumzia tukio hili zinaendelea kufanyika.

error: Content is protected !!