September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kituo cha kuzalisha umeme Mlandizi chateketea

Spread the love

KITUO cha kuzalisha na kusambaza umeme cha Mlandizi mkoani Pwani, kimteketea kwa moto leo tarehe 30 Machi 2019. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI ONLINE kuhusu tukio hilo, Wankyo Nyigesa, Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani amesema, moto huo ulizuka majira ya saa 2.15 asubuhi. 

Kamanda Wankyo amesema, hadi sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana na kwamba, moto huo umeteketeza transform moja yenye megawati 24 ambayo ilikuwa ikizalisha na kusambaza umeme katika maeneo ya Bagamoyo, Kibaha na Mloganzila.

“Nikikuwepo eneo la tukio, hakuna madhara yoyote kwa binadamu isipokuwa jenereta limeteketea.  Hadi sasa chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana, tunasubiri matokeo ya uchunguzi wa watalaamu,” amesema Kamanda Wankyo.


              
            
	          
error: Content is protected !!