February 24, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Chadema wapingwa

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Spread the love

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimepinga vikali kitendo kitendo cha wananchi wanaosadikika ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kujichukulia sheria mkononi kwa kuchoma moto nyumba ya mgombea udiwani aliyehama chama cha Chadema na kujiunga na CCM. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Diwani huyo wa Kata ya Tunduma alikihama chama chake cha Chadema na kujiunga na CCM kwa kile kinachodaiwa kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli.

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga amesema wanakemea kitendo hicho ambacho ni kinyume cha sheria na kuwa kitendo cha kutishia maisha ya mgombea huyo ni tishio kwa haki ya msingi ya kuishi.

“Haki ya mtu kuhama na kujiunga na chama akitalacho ni haki yake anaweza akahama mahali popote, muda wowote na sababu yoyote,” amesema Anna Henga.

Mbali na hilo, Mkurugenzi huyo amesema kuwa kumekuwa na sintofahamu miongoni mwa wananchi katika kata zipatazo 30 ambapo wananchi wamepokwa haki yao ya kushiriki katika uchaguzi mdogo kwa kuenguliwa katika mchakato wa uteuzi wa wagombea kwa madai kuwa hawajui kusoma na kuandika na wengine wakiambiwa kuwa sio raia wa Tanzania.

Henga amesema kuhenguliwa kwa wagombea hao ni kiashiria cha ukiukwaji wa Ibara ya 13 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

error: Content is protected !!