Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko KITS yapeleka Tanzania wawekezaji wa Kimarekani
Habari Mchanganyiko

KITS yapeleka Tanzania wawekezaji wa Kimarekani

Spread the love

 

KAMPUNI ya Kimataifa inayojihusisha na masuala ya Utalii ya Kilimanjaro International Tourism and Safaris (KITS), imeleta wawekezaji wakubwa wawili kutoka Marekani ili kuwekeza nchini Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Wafanyabiashara hao wakubwa Marekani ambao KITS imeratibu safari zao ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Affinity Travel Group, Roslyn Parker na Ofisa Mtendaji Mkuu wa The Pilgram Group, Miguel Pilgram.

Akizungumzia ujio wa wafanyabiashara hao, Mkurugenzi Mtendaji wa KITS, Vonnie Kiondo, amesema, hatua hiyo imefikiwa ili kutekeleza azma ya Serikali ya kuongeza mahusiano ya Kimataifa, uwekezaji na utalii.

Kiondo ambaye ni mmiliki wa Kampuni hiyo, yenye Makao Makuu yake Washington DC, Marekani huku kwa upande wa Tanzania ina ofisi zake Njiro, Arusha, aliwataja

Wageni hao waliwasilia nchini leo Alhamisi na wanatarajia kuondoka nchini tarehe 11 Juni 2021.

Wakiwa nchini Tanzania, wafanyabiashara hao, watafanya mikutano ya uwekezaji katika sekta ya utalii kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Amesema katika ziara ya wageni hao, watakutana na wasanii mbalimbali wa Tanzania ili kuona namna ambavyo wasanii wanaweza kufanya sanaa zao, ikiwemo kutembelea jiji la Dar es Salaam, Wilaya ya Bagamoyo na Zanzibar.

“Tunatarajia ziara hiyo kuwa na faida kubwa na miongoni ni kuuza na kutangaza wasanii na wanamuziki wetu nchini,” amesema Kiondo

Ameongeza “tunatarajia ziara hiyo iweze kuongeza ajira miongoni mwa Watanzania, kuongezeka kwa mapato ya kiuchumi katika sekta mbalimbali zinazohusiana na Utalii na ukarimu ukiwa ni pamoja na kuuzwa nje kwa bidhaa na mavazi ya asili.”

Kiondo amesema, ziara hiyo itanufaisha Tanzania katika ujenzi wa malazi ya gharama nafuu katika maeneo mbalimbali ya hifadhi na yanayotembelewa na wageni wengi ili kufikia lengo la Serikali ililojiwekea la kufikisha jumla ya watalii milioni tano.

Pia, ni kuhakikisha yanakuwepo malazi ya gharama nafuu katika maeneo mbalimbali jambo ambalo litawavutia watalii wengi kutoka Marekani na nchi nyingine duniani kutembelea Tanzania.

Faida nyingine amesema, ni kusaidia Kampuni ya KITS na Watanzania kuchangia ukuaji wa uchumi, mitaji na rasiliamali hivyo wale walio nje ya nchi ni jukumu lao kutangaza nchi na kuleta mitaji nchini.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TTB, Jaji mstafau Thomas Mihayo amesema, anafurahi kupokea ugeni huo kutoka Marekani na watahakikisha wanatoa ushirikiano wa kutoka ili kufikia adhima yao ya kuwekeza.

Kwa upande wake, Pilgram amesema, amefarijika kufika Tanzania “kwani nimekuwa najaribu kuja Tanzania kwa zaidi ya miaka mitano bila mafanikio. Nawashukuru na nafurahi kuwa hapa na nitaona maeneo mengi yenye uwekezaji.”

Akijibu swali la waandishi lililotaka kujua sababu za kushikwa kuja Tanzania kwa miaka mitano, Jaji Mihayo amesema “mimi kwa kweli sijajua alikuwa anakwama wapi.”

Jaji Mihayo amesema, Mama Roslyn anashughulika na watalii wa hali ya juu ambao wanatumia fedha nyingi “mfano wanaweza kuja wachache lakini ndani ya siku moja au mbili wakatumia zaidi ya dola 20,000 na Agosti mwaka huu ataleta watu wengine takriani 20.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wadau wataka kasi iongezeke marekebisho sheria za habari

Spread the love  WADAU wa tasnia ya habari wametakiwa kuongeza juhudi katika...

Habari Mchanganyiko

TEF yawatuliza wadau wa habari marekebisho vifungu kandamizi

Spread the love  JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limewataka wadau wa habari...

Habari Mchanganyiko

Ndege ya Precision Air yaahirisha safari kwa hitilafu, nyingine yatua kwa dharura

Spread the love  NDEGE ya Shirika la Precision Air imeshindwa kufanya safari...

Habari Mchanganyiko

NMB yakabidhi vifaa tiba hospitali Mtwara  

Spread the loveBENKI ya NMB Kanda ya Kusini imetoa msaada wa vifaa...

error: Content is protected !!