August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kitilya, Sioi warejeshwa ‘kitanzini’

Spread the love

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imebatilisha uamuzi wa kufutwa kwa shitaka la utakatishaji fedha lilinaliwakabili Harry Kitilya, Shose Sinare, Sioi Solomon, anaandika Faki Sosi.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Edson Mkwasimongwa Jaji katika mahakama hiyo ambapo amesema kuwa uamuzi uluotolewa awali wa kufuta shitaka hilo ni haikuwa sahihi.

Kitiliya, alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato hapa nchini (TRA); huku Sinare akiwa Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji na Sioi akiwa Mwanasheria wa Benki ya Stanbic Tawi la Tanzania.

Awali uamuzi huo ulifanywa na Amillis Mchauru Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Kisutu 27 Aprili mwaka huu baada ya kusikiliza pande zote mbili na kudai kuwa shitaka hilo lina upungufu kisheria unaofanya lisijitosheleze.

Upande wa mashitaka ulikata rufaa ya kupinga uamuzi huo na kutafuta suluhu ya kisheria hatimaye leo uamuzi huo umebatishwa.

Hapo awali, watuhumiwa hao walipandishwa kizimbani tarehe 1 Aprili na kusomewa mashitaka nane yakiwemo ya kughushi nyaraka, kutengeneza mkataba bandia kupitia kampuni ya udalili ya Enterprise Growth Market Advisor (EGMA);

Pamoja na shitaka la utakatishaji fedha kiasi cha dola milioni mia sita za kimarekani.

Kwa sasa jalada la kesi hiyo litarudishwa tena katika mahamakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na ili kutoa nafasi kwa kesi hiyo kuendelea kusikilizwa huko.

error: Content is protected !!