July 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kitilya, Sinare, Sioi wachekelea

Spread the love

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam imekataa rufaa ya kupinga kufutwa kwa shitaka la nane katika kesi inayowakabili Harry Kitilya, Shose Sinare, Sioi Solomoni, anaandika Faki Sosi.

Shitaka la nane katika kesi hiyo ni la utakatissji fedha ambalo lilifutwa na Amilis Mchauru katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyosababisha upande wa mashitaka kutoridhika na uamuzi huo.

Kitiliya, alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA); Sinare, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji na Sioi, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic Tawi la Tanzania.

Akitoa uamuzi huo Moses Mzuna, Hakimu Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam amesema kuwa, rufaa hiyo haina mashiko kisheria.

“Rufaa ya shitaka hili haina miguu” amesema Hakimu Mzuna wakati akitoa uamuzi wa rufaa hiyo.

Hakimu Mzuna amesema kuwa, hoja ya upande wa utetezi ya kueleza kuwa, Mahakama Kuu haina mamlaka ya kusikiliza rufaa hiyo kutokana kesi hiyo bado haijafika mwisho na kwamba, Mahakama ya Kisutu iliweza kusikiliza kesi hiyo.

Hakimu Mzuna amefuta rufaa hiyo na kwamba, kesi hiyo itaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Hakimu Mzuna amemshauri Timon Vitalis, Wakili Mkuu wa Serikali kuendelea na kesi hiyo na kwamba, endapo kesi itafika mwisho wakiwa hawajridhika na uamuzi, wanaruhusiwa kukataa rufaa.

Hata hivyo Mzuna amesema kuwa, upende wa mashitaka wanayo mamlaka ya kubadili hati ya mashtaka.

Hata hivyo, Vitalis amesema kuwa, wamepokea uamuzi wa Mahakama Kuu lakini atakata rufaa katika Mahakama ya Rufani.

Ndugu wa washitakiwa walionekana wakitoa machozi kwa furaha walipotoka nje ya Mahakama Kuu kutokana na kufutwa kwa rufaa hiyo.

error: Content is protected !!