May 16, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kitillya, wenzake: Faini Bil 1.5 au jela miezi sita

Spread the love

MAHAKAMA Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi nchini Tanzania, imemhukumu Harry Kitillya, aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na wenzake kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya Shilingi 1.5 Bilioni. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Washtakiwa wengine kwenye shauri hilo ni pamoja na Shose Sinare, Sioi Solomon, Bedason Shallanda na Alfred Misana. Kwa pamoja washtakiwa hao walikiri makosa yao.

Shose ni alikuwa Ofisa wa Kitengo cha Uwekezaji kwenye benki ya Stanbick pia alikuwa Miss Tanzania 1996, Solomon alikuwa Mwanasheria wa Benki hiyo.

Shallanda alikuwa Ofisa wa Sera kwenye Wizara ya Fedha za uchumi, Misana akiwa Kamishana msaidizi Kitengo cha Madeni kwenye idara ya Sera wizarani hapo.

Washtakiwa hao walikubali kulipa faini hiyo ambapo kila mmoja alitakiwa kulipa Sh. 1 Mil kutoka na kesi ya uhujumu uchumi inawakabili. Hukumu hiyo imetolewa jana Jumanne tarehe 25 Agosti 2020 na jaji wa mahakama hiyo, Immaculate Banzi.

Washtakiwa hao walifutiwa mashtaka 57 na kubaki shitaka moja la kuisababishia serikali hasara kiasi cha Dola za Marekani milioni 600. Kesi hiyo ilianza kupitiwa jana saa 11 na kuisha saa 2 usiku.

Washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Machi 2013 na Septemba 2015, wakati wa mchakato wa mkopo wa Dola za Marekani milioni 550 kwa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard ya Uingereza.

Aidha, wanadaiwa kula njama za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ili kujinufaisha wenyewe na washirika wao. Kwenye kesi hiyo, mawakili wa washtakiwa walikuwa Alex Mgongolwa na Jeremiah Mtobesya.

error: Content is protected !!