July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kitillya, Sinare wang’ang’aniwa

Spread the love

 

KABLA ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kuondoa shitaka la utakatishaji fedha katika kesi inayowakabili Harry Kitillya, Shose Sinare na Sioi Solomoni, upande wa mashitaka umekata rufaa ya kupinga mwelekeo wa kuondolewa kwa shitaka hilo, anaandika Faki Sosi.

Kitillya, alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA); Sinare, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwezekezaji katika Benki ya Stanbic na Sioi Solomoni, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic.

Amilis Mchaura, Hakimu Mkazi Kisutu amesema kuwa, shitaka la nane linalowakabili watuhumiwa hao lina upungufu kisheria hivyo mahakama italifuta shitaka hilo.
Jopo la mawakili wa upande wa utetezi linaongozwa na Dk. Lingo Tenga liliomba mahakama kuwapa wateja wao dhamana yenye masharti nafuu.

Baada ya Amilis Mchaura, Hakimu Mkazi  kusimamisha kusikiliza kesi hiyo kwa dakika 30, aliporejea tu, Oswadi Tibabyekonya, Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali alileta notisi ya rufaa kutoka Mahakama Kuu iliyokuwa ikipinga mwelekeo wa kufutwa kwa shitaka la utakatishaji fedha.

Hakimu Mchaura baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, alihalisha shauri hilo na kwamba, uamuzi atautoa tarehe 29 Aprili mwaka huu. Watuhumiwa wote wamekosa dhamana wamerudishwa rumande.

 

error: Content is protected !!