September 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kitillya, Sinare wabanwa kortini

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imepuuza ombi la dhamana ya kesi inayowakabili Harry Kitillya, Shose Sinare na Sioi Solomoni ambapo wamerejeshwa rumande, anaandika Faki Sosi.

Kitillya, alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA); Sinare, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwezekezaji katika Benki ya Stanbic na Sioi Solomoni, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic.

Dhamana yao imesikilizwa mbele ya Amilis Mchaura, Hakimu Mkazi Kisutu ambazo mawakili wa pande zote mbili waliwasilisha hoja zao.

Dk. Lingo Tenga ndiye aliyeongoza jopo la mawakili upande wa watetezi ambapo upande wa serikali umesimamiwa na Oswadi Tibabyekonya, Wakili Mkuu wa Serikali Mahakama ya Kisutu.

Upande wa utetezi uliomba mahakama kubatilisha mashitaka ya utakatishaji pesa haramu ulisababisha watuhumiwa hao kukosa dhamana. Tibabyekonya ameieleza mahakama kuwa, mashitaka la utakatishaji fedha hayana dhamana.

Upande wa utetezi ulifanya mapitio ya kesi mbalimbali zinazofanana na kesi hizo ikiwemo kesi namba 314 ya mwaka 2015 kwenye Mahakama ya Rufaa ya Mwanza iliyokuwa ikimkabili Kigunda Francis aliyeshitakiwa kwa kosa kama hilo lakini alipewa dhamana.

Christopher Msigwa, wakili wa serikali amesema kuwa kesi hiyo haina dhamana kwa sababu, kosa hilo linaathiri uchumi wa taifa.

Washitakiwa wamekosa dhamana na wamerudishwa rumande hadi tarehe 22 Aprili mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

error: Content is protected !!