August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kitillya na wenzake wataka upelelezi uharakishwe

Spread the love

UPANDE wa utetezi katika kesi inayowakabili Harry Kitillya, aliyekuwa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shose Sinare, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwezekezaji katika Benki ya Stanbic na Sioi Solomoni, mwanasheria wa benki hiyo, umeutaka upande wa Jamhuri kuwahisha upelelezi, anaandika Faki Sosi.

Alex Mgongolwa, wakili wa watuhumiwa hao. Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Respecious Mkeha amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo una muda wa miezi sita bila kukamilika.

Awali, wakili wa serikali Kishenyi Mutalemwa alidai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na kwamba Mkurugenzi wa Mashtaka ameeleza kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) inaendelea na upelelezi.

Hakimu Mkeha ameitaka Jamhuri kukamilisha Upelelezi wa shauri hilo kwa wakati huku akitangaza kuahirisha kesi hiyo mpaka terehe 4 Novomba, Mwaka huu.

Watuhumiwa hao walipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo kwa kosa la kuhujumu uchumi wakidaiwa kughushi nyaraka na kufanikisha uhalifu huo kati Agosti 2012 na Machi 2013 jijini Dar es Salaam.

Kosa la pili, linadaiwa kufanywa na Sinare, tarehe 2 Agosti mwaka 2012 kwa kughushi hati ya mkopo wa Dola za Marekani 550 milioni katika Benki ya Stanbic ya Tanzania na Benki ya Standard ya Uingereza akiiombea fedha Serikali ya Tanzania.

Sinare anatuhumiwa kwa kosa la tatu alilotenda tarehe 13 Agosti 2012, la kupeleka hati ya kughushi kwenye Wizara ya Fedha iliyoonesha kuwa Serikali ya Tanzania itapewa mkopo wa Dola za Marekani 550 milioni kutoka Benki ya Stanbic ya Tanzania na Standard ya Uingereza.

Washitakiwa hao pia wote wanakabiliwa na kosa la kutengeneza mkataba bandia tarehe 5 Novemba, mwaka 2012 jijini Dar es Salaam katika Makao Makuu ya Benki ya Stanbic kupitia Kampuni ya Enterprise Growth Market Advisor (EGM).

Shitaka lingine linalowakabili watuhumiwa wote ni utakatishaji fedha wanalodaiwa kulitenda kati ya mwezi Machi 2013 na Septemba 2015.

error: Content is protected !!