July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kitete cha simu ‘feki’ chaanza

Spread the love

BAADHI ya wafanyabiashara nchini mwameanza kupaza sauti kwamba, muda uliowekwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kuzifungia mawasiliano simu feki ni mfupi, anaandika Dany Tibason.

Hivi karibuni TCRA wameetoa taarifa kwamba ifikapo Juni mwaka huu, simu ambazo si halisi ‘feki’ hazitaweza kufanya kazi na kuwataka wananchi kuanza kuchunguza simu zao na kisha kurejesha walipozinunua ama kujiandaa kununua mpya na halisi.

Placid Nkya, mmilikiwa wa duka la simu la ‘Kwa Pablo’ mkoani Dodoma akizungumza na Mwanahalisi Online ameiomba serikali kuongeza muda wa kuzima simu feki kwani muda uliotangazwa ni mfupi huku akidai Watanzania walio wengi hawana elimu ya kutosha.

Amesema, wananchi wengi wamekuwa wakinunua simu maarufu kama ‘za kichini’ kutokana na kuwa ni za gharama nafuu na hivyo walionunua kuingia hasara.

“Kwao ni hasara kwa kuwa, bado simu inatumika na wala haijaharibika lakini mtu anatakiwa kununua nyingine. Kwanini wasianze kudhibiti kule zinakotoka ili kuwanusuru wananchi na gharama hizi?” amehoji.

Mfanyabiashara John Koyanga anaelekeza lawama zake kwa TCRA kwa kutochukua hatua hizo tangu mapema ili kuhakikisha wananchi hawapati hasara ya kununua na kuzitumia kwa muda mchache na kisha kufungwa.

Pia amelaumu Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na serikali kwa uzembe wa kushindwa kuzuia uingizwaji wa simu zisizofaa na badala yake serikali ikaiwa inaendelea kukusanya kodi kwenye maduka yanayouza simu hizo.

Kiyanga amesema, kwa sasa wauzaji wa simu wamekuwa wakikumbana na usumbufu mkubwa kwa wateja wao ambao wamekuwa wakirudisha simu kwa madai ya kwamba ni feki.

“Sisi tunauza simu na kiukweli simu hizo zinazodaiwa kuwa ni feki zinauzwa kwa bei nafuu kutokana na kipato alichonacho mteja.

“Lakini kiukweli iwapo zitaanza kuuzwa simu ambazo zinaonekana kuwa ni halisi watu wengi watashindwa kununua kwani simu nyingi zitakuwa zikiuzwa kwa bei ghali zaidi,” amesema Koyanga.

error: Content is protected !!