November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kitendawili cha Muswaada wa Vyama vya Siasa kuteguliwa

Bunge la Tanzania

Spread the love

LEO MKUTANO wa kumi na nne Bunge la kumi na moja linatarajiwa kuanza shughuli zake jijini Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kwa mujibu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kimataifa Ofisi ya Bunge kimeeleza kuwa kati ya shughuli zitakazofanywa ni pamoja na bunge kujadili na kupitisha miswaada mitano ya sheria ambayo itasomwa kwa hatua ya pili na ya tatu.

Kitengo hicho kimesema kuwa miswada itakayojadiliwa ni Muswaada wa Sheria ya Marekebisho ya vyama vya siasa wa mwaka 2018, Muswaada wa Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wa mwaka 2018.

Muswaada mwingine ambao utajadiliwa ni Muswaada wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti na Usafi wa Ardhi wa mwaka 2018, Muswaada wa Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira wa mwaka 2018 pamoja na Muswaada wa Sheria ya Marekebisho ya sheria mbalimbali (Na4) wa mwaka 2018.

Aidha katika mkutano wa kumi na nne wa Bunge Kamati za kudumu za bunge zitawasilisha taarifa za mwaka za kazi za kamati hizo kwa mujibu wa masharti ya kanuni ya 117(15) kanuni za Bunge.

Kamati hizo ni Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Kamati ya huduma ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Kamati ya Kudumu ya Bunge Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, Kamati ya Kudumu ya Bunge la Bajeti, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira.

Kamati nyingine ni Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji.

Kitengo hicho pia kilizitaja kamati nyingine kuwa ni Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Shughuli nyingine zitakazo fanyika ni pamoja na Kiapo cha Uaminifu kwa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abdallah Ally Mtolea (CCM) pamoja na maswali wastani wa maswali 125 ya Kawaida yanatarajiwa kuulizwa na Wabunge.

Aidha, wastani wa Maswali 16 ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yanatarajiwa kuulizwa kwa siku za Alhamisi tarehe 31 Januari, na 7 Januari, 2019.

error: Content is protected !!