April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kitachofanywa na JPM siku tano za ziara yake Dodoma

Jiji la Dodoma

Spread the love

RAIS John Magufuli anatarajiwa kufanya ziara ya siku tano jijini Dodoma, kuanzia tarehe 21 – 25 Novemba 2019. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari, leo tarehe 20 Novemba 2019, Dk. Binilith Mahenge, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amesema, Rais Magufuli atatembelea miradi inayotekelezwa kwenye jiji hilo.

Amesema, miongoni mwa shughuli atazofanya Rais Magufuli ni pamoja na kuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 10 katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), siku ya Alhamisi tarehe 21 Novemba mwaka huu.

Dk. Mahenge amesema, Ijumaa ya tarehe 22 Novemba 2019, atatembelea na kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa Hospitali ya Uhuru Wilayani Chamwino, Ujenzi wa Nyumba 118 za polisi katika maeneo ya FFU Nzuguni na Medel East.

Pia ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Stendi Kuu ya mabasi iliyopo Nzuguni na Soko Kuu linalojengwa katika eneo la Nzuguni.

Amesema, tarehe 25 Novemba 2019, Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) – Kikombo, ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji na Ujenzi wa Jengo la Makandarasi eneo la National Capital City.

Na kwamba, maandalizi ya ziara hiyo yamekamilika, ambapo ametoa wito kwa wananchi wote kujitokeza ili kumsikiliza Rais Magufuli.

error: Content is protected !!