May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kitabu ‘Safari ya Maisha Yangu’ cha Mzee Mwinyi kuzinduliwa

Spread the love

 

MZEE Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania, anatarajia kuzindua tawasifu kuhusu maisha yake, Jumamosi ijayo tarehe 8 Mei 2021. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa na Mtoto wa Mzee Mwinyi, Dk. Hussein Mwinyi kupitia ukurasa wake wa Twitter, leo tarehe 2 Mei 2021.

Dk. Hussein ambaye ni Rais wa Zanzibar, amesema kitabu hicho kimebeba simulizi ya maisha ya Mzee Mwinyi katika uongozi na siasa.

“Tawasifu ya Rais wa Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Ali Hassan Mwinyi iitwayo ‘Mzee Rukhsa: Safari ya Maisha Yangu’ itazinduliwa tarehe 8 Mei 2021. Kitabu hiki kimebeba simulizi za maisha yake binafsi na safari yake ya uongozi,” ameandika Rais Hussein.

Uzinduzi huo wa tawasifu ya Mzee Mwinyi aliyeiongoza Tanzania kwa mihula miwili mfululizo (1985-1995), utafanyika jijini Dar es Salaam. Mzee Mwinyi alizaliwa tarehe 8 Mei 1925, Kivule, Dar es Salaam.

error: Content is protected !!