WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amesema Serikali inaendelea na mapamba dhidi ya wala rushwa na haitawaacha salama viongozi wala rushwa na mafisadi ambao wamekuwa wakitumia vibaya fedha za umma na kukwamisha miradi ya maendeleo ya wananchi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).
Majaliwa, ameyasema hayo leo Alhamisi tarehe 14 Januari 2021, jijini Dodoma wakati alipokuwa akizindua kitabu kinachohusu utendaji kazi wa Rais John Magufuli, katika awamu ya kwanza ya miaka mitano ya uongozi wake kinachoitwa ‘The Game Changer’, President Magufuli’s First Term in Office.
Amesema, Serikali ya awamu ya tano itaendeleza mapambano dhidi ya viongozi wala rushwa na mafisadi wa fedha za umma ambao wamekuwa wakitamani siku zote kujinufaisha wao na siyo wananchi wanyonge.
“Mapambano dhidi ya wala rushwa yanaendelea pamoja na viongozi mafisadi ambao wamekuwa na tabia ya kula fedha za umma na kusababisha miradi ya mendeleo kukwama na wananchi kuendelea kupata shida katika maeneo yao,” amesema Majaliwa.
Majaliwa amesmea, Tanzania kufikia asilimia 98 ya kupinga rushwa inawezakana kama kila mmoja atatimiza wajibu wake katika kuhakikisha rushwa inakua haina nafasi katika taifa nzima,” amesema
“Watu ambao wanadhani watatajirika kupitia rushwa mawazo hayo wayafute vichwani mwao kwani serikali hii itaendeleza mapambano dhidi ya rushwa na hakuna kiongozi atakayeachwa salama katika suala hili,” amesema Majaliwa.
Aidha, amewataka wananchi kuisadia serikali katika mapambo dhidi ya rushwa, kwa kuwafichua wote ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo hivyo ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Sambamba na hilo, amesema, hivi sasa wanafanyia kazi maagizo ya Rais Magufuli, aliyoyatoa wakati akizindua Bunge la 12 mwishoni mwa mwaka 2020.
Moja maagizo hayo, alisema ni pamoja na kuondoa vikwazo kwa wawekezaji wenye nia ya kutaka kuwekeza nchini kupata vibali ndani ya siku 14.
Akizungumzi kitabu hicho, Majaliwa amesema, taasisi zote za umma zinatakiwa kuwa nacho ili kuwa msaada katika utekelezaji wa majukumu yao.
“Kitabu hichi kimesheheni mambo mbalimbali ambayo yamefanyika katika awamu ya kwanza ya utawala wa Rais Magufuli, ambapo ndani yake yameongelewa mambo mbalimbali kama vile mapambano ndhidi ya rushwa, ufisadi, pia kimegusia sera na dira ya taifa letu katika kufikia uchumi wa kat,i” amebainisha Majaliwa
Akitoa maelezo kuhusu kitabu hicho, Mhariri mkuu, Profesa Ted Maliyamkono alisema, kimeandikwa na watu wasiopungua 47, huku kikihusisha wataalum kutoka vyuo mbalimbali kama vile, Vyuo Vikuu vya UDOM, UDSM, IFM, Mipango pamoja na taasisi nyingine za serikali kikiratibiwa na Taasi ya utafiti vyuo vikuu Masahariki na kusini mwa Afrika (ESAURP).
Prof, Maliayamkono alisema, kitabu hicho kimechambua namna ambavyo Rais Magufuli, amekuwa mwanabadiliko kwa kubadilisha mifumo mbalimbali ndani ya serikali katika kipindi chake cha kwanza cha utawala.
“Katika kipindi chake cha kwanza tumeshuhudia mikataba mibovu ikikataliwa kama ule wa ujenzi wa SGR na kampuni ya Kichina, ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ambao mkataba wake ulikuwa hauna faidida na Taifa pia katika kipindi chake ulikataliwa lakini pia ameboresha mikataba ya madini na hivi sasa faida inayopatikana tunagawana asilimia 50 kwa 50 na makampuni ya uchimbaji madini,” alifafanua Profesa Maliyamkono
Leave a comment