Monday , 27 May 2024
Home Sports Kisinda hati hati kuikosa Azam Fc
Sports

Kisinda hati hati kuikosa Azam Fc

Spread the love

 

Winga wa klabu ya Yanga Tuisila Kisinda huwenda akaukosa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam Fc mara baada ya kupata majeruhi kwenye mchezo uliopita dhidi ya Gwambina FC. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo dhidi ya Azam Fc utapigwa kesho kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa 2:15 usiku.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habairi hii leo kwenye makao makuu ya shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF, kuelekea mchezo wa kesho kocha wa makipa wa klabu ya Yanga Razak Siwa ameleza kuwa kuelekea mchezo huo atakosa huduma ya Mapinduzi Barama ambaye bado hajapona ila Tuisila Kisinda bado yupo hati hati.

https://www.youtube.com/watch?v=RM9dFsdSxnY

“Kuelekea mchezo wa kesho tutamkosa Mapinduzi Balama na Kisinda ambaye yupo hati hati ila wengine wote wapo tayari kwa mchezo wa kesho” alisema kocha huyo

Kisinda alipata majeruhi ya bega kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu dhidi ya Gwambina ambao Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa kwenye dimba la Azam Complex Chamazi Yanga ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 1-0.

Mpaka sasa Yanga ipo kileleni ikiwa mna pointi 57 nyuma ya pointi mbili kwa Simba ambao wanapointi 55, wakitofautiana michezo mitatu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Sports

The COVID Data That Are Actually Useful Now

Spread the loveMauris mattis auctor cursus. Phasellus tellus tellus, imperdiet ut imperdiet...

Sports

The No Sugar Challenge That Almost Broke Me

Spread the loveMauris mattis auctor cursus. Phasellus tellus tellus, imperdiet ut imperdiet...

Sports

The Unorthodox Solution to the World’s Migration Woes

Spread the loveMauris mattis auctor cursus. Phasellus tellus tellus, imperdiet ut imperdiet...

Sports

How To Season 3: When Expectations Don’t Meet Reality

Spread the loveMauris mattis auctor cursus. Phasellus tellus tellus, imperdiet ut imperdiet...

error: Content is protected !!