Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Biashara Kishindo fainali NMB MastaBata, 30 wajinyakulia Mil. 90
Biashara

Kishindo fainali NMB MastaBata, 30 wajinyakulia Mil. 90

Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi Benki ya NMB, Aikansia Muro akibonyeza kitufe kuashiria kuchezesha Droo ya mwisho ya msimu wa tatu wa Kampeni ya NMB MastaBata Kivyako Vyako, wakati wa droo hiyo iliyochezeshwa katika Tawi la NMB Sinza Mori jijini Dar es Salaam jana.
Spread the love

MIEZI mitatu ya Kampeni ya ‘NMB MastaBata – Kivyako Vyako,’ iliyoendeshwa na benki hiyo, imefikia tamati kwa washindi 30 kujinyakulia Sh.3 milioni kila mmoja. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Droo hiyo imehitimishwa leo Jumatano, tarehe 23 Machi 2022 ambayo imefanyikia NMB Tawi la Sinza jijini Dar es Salaam.

Jumatano Machi 23 kwa wateja 30 kujinyakulia kitita cha Sh. Mil. 90 (sawa na Mil. 3 kila mmoja), hivyo kukamilisha kinyang’anyiro kilichobeba zawadi ya pesa taslimu Sh.240 milioni.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya Nmb, Filbert Mponzi (wa tatu kulia) akibonyeza kitufe kuashiria kuchezesha Droo ya mwisho ya msimu wa tatu wa Kampeni ya NMB MastaBata Kivyako Vyako, wakati wa droo hiyo iliyochezeshwa katika Tawi la NMB Sinza Mori jijini Dar es Salaam jana.

Hitimisho ‘Grand Finale’ la kampeni hiyo, limefanyika NMB Tawi la Sinza jijini Dar es Salaam, kufikia ukomo kwa mchakato uliowanufaisha wateja 1,080, kati yao 1,000 wakijinyakulia Sh.100 milioni 100 (sawa na Sh. 100,000 kila mmoja), huku 50 wakitwaa Sh.50 milioni sawa na Sh.1 milioni kila mmoja na 30 wa fainali wakishinda Sh.90 milioni.

Akizungumza kabla ya droo ya fainali hiyo, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, amesema malengo ya kampeni hiyo, ambayo ni kuhamasisha matumizi ya kadi badala ya pesa taslimu, yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa na kwamba kutamatika kwa NMB MastaBata ni mwanzo wa ujio wa kampeni nyingine.

“Tuko hapa kuhitimisha kampeni iliyoanza Desemba 2021, ikilenga kuhamasisha wateja kutumia kadi katika kufanya malipo. Matumizi ya pesa taslimu yapo, ila tunapaswa kuyapunguza kwa sababu za kiusalama. Tunatumia nguvu kubwa katika kuhamasisha wateja kutumia kadi za MasterCard kufanya malipo yoyote, bila kuwa na pesa taslimu,” amesema Mponzi.

Balozi wa Kampeni hiyo, Masoud Kipanya (wa pili kulia) akipiga simu kwa mmoja kati ya wateja waliobahatika kushinda na kujinyakulia kitita cha sh. milioni tatu, wakati wa kuchezesha droo ya mwisho ya msimu wa tatu wa Kampeni ya NMB MastaBata Kivyako Vyako, iliyochezeshwa katika Tawi la NMB Sinza Mori jijini Dar es Salaam jana.

“Kampeni hii ya miezi mitatu, imetoa zawadi za pesa kiasi cha Sh.240 milioni, tumeshatoa Sh.150 milioni na leo tunatoa Sh.90 milioni kwa wateja 30. Hii inamaanisha kuwa NMB inatambua thamani ya matumizi ya kadi badala ya pesa taslimu, kwa kuwazawadia wateja wanaofanya hivyo.”

Mponzi amesema, “pesa zilizotolewa kwa wateja ni kama motisha yetu kwao, kwamba wamefanya manunuzi kwa faida zao wenyewe, lakini sisi kama benki tukaona tuwazawadie katika kuchagiza matumizi yasiyohusisha pesa taslimu,” alisisitiza Mponzi mbele ya wanahabari na wageni waalikwa.”

Ameongeza, “kampeni hizi hazijakoma, zitaendelea na tutaendelea kutoa elimu kwa jamii itambue umuhimu wa mabadiliko, kwa sababu matumizi ya kadi ni rahisi, nafuu na salama zaidi. Kampeni imekuwa na mafanikio na kumekuwa na ongezeko la asilimia 10 la watumiaji wa kadi.”

“Na kwa sababu kampeni kama hizi zitakuwa endelevu, basi wito wetu kwa Watanzania wasio na akaunti ni kufungua haraka iwezekanavyo na wale wateja wetu waendelee kuweka akiba ili kuwa wanufaika wa masuuhishi mbalimbali na kihuduma tunayotoa NMB” aliongeza Mponzi.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Elibariki Sengasenga, amepongeza aina ya ushirikiano baina ya NMB na Bodi yake, tangu kuanza kwa kampeni hiyo Desemba mwaka jana walipoenda kwao kuomba leseni ya kuendesha droo za kampeni hiyo.

“Pongezi kwenu NMB kwa kufuata taratibu, kuja kwetu kuomba leseni ya kuendesha kampeni hii na kila droo mkahakikisha kunakuwa na mwakilishi wetu. Kwa kipindi chote, hatukupokea malalamiko yoyote. Ilikuwa ni kampeni rahisi kwa mteja kushiriki, ile kufanya tu matumizi yako mwenyewe na kwa faida zako, unajikuta katika nafasi ya kuzawadiwa.

“Na jambo la kufurahisha zaidi, idadi ya washindi ilikuwa ni kubwa mno, hivyo wanufaika walikuwa wengi. Mngeweza kubuni shindano dogo lenye kuwazawadia wateja wachache, ila mkaona hapana, muwafikie wengi zaidi, hili ni jambo la kupongezwa,” amesema Sengasenga, ambaye aliomba kuwe na muendelezo wa kampeni kama hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari

Bosi utalii atoa ujumbe wa mikopo nafuu ya NMB

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini...

BiasharaHabari

NMB yavutia wabunifu suluhisho za kifedha, Dk. Mpango agusia vijana

Spread the love  MFUMO wa majaribio wa suluhishi za kifedha ulioandaliwa na...

BiasharaHabari

NMB Nuru Yangu yazinduliwa, 200 kunufaika

Spread the loveBENKI ya NMB nchini Tanzania imetangaza rasmi kuanza kupokea maombi...

BiasharaHabari

Waziri Bashe uso kwa uso vigogo NMB bungeni

Spread the loveWAZIRI wa Kilimo nchini Tanzania, Hussein Bashe amekutana na kufanya...

error: Content is protected !!