April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kishindo cha Zitto; Sina hofu ya vitisho

Spread the love

HOFU anayojengewa Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, ndani na nje ya Bunge haimyumbishi. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea). Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam …(endelea).

Amesema, licha ya vitisho dhidi yake wakati akiwa ziarani Marekani, amerudi nchini bila hofu na hakuna wa kunifanya chochote.

Akizungumza na waandishi wa habari usiku wa tarehe 17 Februari 2020, muda mchache baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam, amesema ametekeleza wajibu wake kama mwasiasa.

“Sina hofu yoyote, ndio maana nimerudi bila shida yoyote kwa sababu hakuna kosa nililofanya.

“Nimetekeleza wajibu wangu kama kiongozi wa kisiasa mimi mbunge,” amesema Zitto.

Kiongozi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema, Tanzania ni nchi ya vyama vingi hivyo Watanzania wawe tayari kukinzana kimawazo na mitazamo.

“Watanzania wafahamu kuwa nchi yetu ya vyama vingi, na ni lazima kuwe na tofauti za kimawazo, tofauti za mikakati na tofauti za mitazamo,” amesema na kuongeza:

“Inatakiwa wanasiasa baadala ya kutumia dola ama vitisho, tushindane kwenye hoja.”

Pia amesema, hawezi kukimbia vitisho wala kuingiwa na badala yake atavikabili.

“Hapajawahi kuwa na nyakati ambayo wata wanahofu ya mawazo kama kipindi hiki.

“Sasa huiondoi hofu kwa kuikimbia, unaiondoa kwa kuikabili, ndio maana mimi licha ya vitisho vyote nilivyopewa, nimewaambia nitarudi nchini na nimerudi nchi na hakuna chochote watakachoweza kunifanya,” amesema.

Akizungumzia ziara yake ya Marekani amesema, imekuwa na manufaa makubwa kwa Demokrasia.

“Ziara yangu ilikuwa inamafanikio makubwa, ndio maana watawala wanahangaika na wanaendelea na vitisho kwa sababu ya mafanikio niliyoyapata kwenye ziara yangu,” amesema.

error: Content is protected !!