Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kishimba ampa tano Rais Samia kutoa tani 1000 Kaham Mjini
Habari za Siasa

Kishimba ampa tano Rais Samia kutoa tani 1000 Kaham Mjini

Mbunge wa Kahama Mjini, Jumanne Kishimba (CCM)
Spread the love

 

MBUNGE wa Kahama Mjini, Jumanne Kishimba (CCM) amesema wameaza kupokea tani 100 mahindi kwa ajili ya chakula na wataendelea kupokea tani zingine 1,000 ambazo zitasaidia wananchi kwa kipindi hiki ambacho bado kuna changamoto ya chakula. Anaripoti Paul Kayanda, Kahama … (endelea).

Amesema wananchi wa Kahama wanamshukuri Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake kuhakikisha wananchi kupata chakula kitakachowasaidia kwa kipindi hiki ambacho wanatarajia kwenda kuvuna mazao miezi ijayo.

Kishimba ameyasema hayo jana tarehe 10 Januari, 2022 wilayani Kahama wakati akishuhudia wananchi wakinunua mahindi kwa bei elekezi ya Serikali ya Sh 15,000 kwa debe moja lenye ujazo wa kilo 20.
Amesema bei hiyo inasaidia kupunguza mfumuko wa bei mitaani hususani kwenye maeneo ya Luzewe, Katoro mkoani Geita pamoja na Kagongwa wilayani humo ambalo wanalima mahindi kwa wingi.

“Tunaomba wananchi wa maeneo mengine ambako wataanza kupeleka Mahindi siku chache zijazo wawe wavumilivu lakini pia kama wataweza kuja hapa Kahama Mjini itakuwa vizuri,” amesema Kishimba.

Mbunge huyo amekiri kwamba hali ya chakula kwa wananchi wa jimbo ilikuwa mbaya kwa sababu debe moja la mahindi lilikuwa linauzwa kwa bei ya Sh 25000 ambayo ni bei ya juu kuwahi kuishuhudia.
Amesema baada ya Serikali kuleta ahueni ya bei ya mahindi kwa wananchi mitaani bei imeaza kupungua na hiyo ni baada ya wafanyabiashara kugundua kuwa Serikali imeaza kuleta mahindi kwa wananchi wake.

“Kutokana na hali hii tunatarajia inaweza kutusaidia kabla hatujapata chakula kingine kwa maana ya kuvuna hivyo tunaendelea kuwahimiza wananchi wajikite zaidi kwenye uzalishaji hasa wakati huu ambao mvua zinaendelea kunyesha na kwa sababu wananchi wa jimbo hili ni wachapa kazi,” amesema Kishimba.

Hata hivyo, amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa nchini na kuviomba vyama vyote kutumia fursa hiyo kuelezea mazuri yanayofanywa na Serikali lakini pia kueleza sera zao mbele ya wananchi.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

error: Content is protected !!