Tuesday , 27 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Kisena, wenzake 3 wafikishwa kizimbani na kusomewa mashtaka 33
Habari MchanganyikoTangulizi

Kisena, wenzake 3 wafikishwa kizimbani na kusomewa mashtaka 33

Spread the love

ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (UDART), Robert Kisena na wenzake watatu wamesomewa mashataka 15 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo tarehe 9 Mei, 2022 ikiwemo utakatishasji wa fedha kiasi cha 750 milioni kwenye kesi namba 21 ya Mwaka 2022.

Pia amesomewa mashtaka 18 na wenzake wawili ikiwemo kusababishia hasara Serikali kiasi cha Sh bilioni 5.2 kwenye kesi namba 20 ya mwaka 2022. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Washtakiwa hao wamesomewa kesi mbili tofauti za uhujumu uchumi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Godfrey Issaya na Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na jopo la mawakili watano wandaamizi wa Serikali wakiongozwa na Pius Hilla akisaidiana na Jackline Nyatori, Ester Martin, Iman Mitumemingi na Upendo Temu, wamewataja washtakiwa wengine mbali na Kisena kuwa ni Charles Newe (48) Mkurugenzi wa Udart, mfanyabiashara John Samangu (66) na Mtunza fedha Tumaini Kulwa (44).

Mbele ya Hakimu Issaya,  Wakili wa Serikali Mwandamizi, Jackline Nyantore amedai washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 18 ikiwamo kuongoza genge la uhalifu linalowakabili washtakiwa, Kisena, Newe na Kulwa.

Mashtaka  manne ya kughushi, mashtaka manne ya kuwasiliana nyaraka za uongo, mashtaka nane ya  utakatishaji fedha na moja la  kuisababishia hasara mamlaka hiyo.

Wakili Nyotori amedai kuwa washtakiwa watatu wanadaiwa kutenda kosa la kuongoza genge la uhalifu ambapo inadaiwa kuwa kati tarehe 1 Agosti 2015 na tarehe 30 Desemba 2015 katika jiji la Dar es Salaam waliongoza genge la uhalifu kwa lengo la kujipatia  sh bilioni 4.5 kutoka shirika la Usafiri Dar es Salaam Dart kupitia kwenye akaunti ya Benki namba 20110017710 ya Benki NMB tawi  la Bank House jijini Dar es Salaam.

Shaka la pili linawahusu Kisena na Newe ambapo wanadaiwa tarehe 1 Juni 2015 na 30 Aprili 2016 katika wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam washtakiwa walighushi nyaraka  yenye jina la Intelligent Transportion System (ITS) ambayo iliyonesha kuwa UDART  wameingia mkataba na Maxcom Limeted tarehe 20 Juni 2015 wa kusambaza kadi za Near Field  Communications  Card (NFC) yenye thamani ya Sh bilioni 2.2 wakijua kuwa wanadanganya.

Shitaka la tatu nne na tano  linamhusu mshtakiwa Newe  ambapo anadaiwa tarehe 9, 12 Novemba 2015 akiwa National  Microfince Bank  Ilala jijini Dar es Salaam alighushi  nyaraka za uongo na kujipatia kiasi cha bilioni 2.2 huku  kwenye shitaka la sita  na la saba kwa njia hizo hizo alijipatia kiasi cha 3.5 huku akijua kuwa amelaghai.

Shitaka la Nane na tisa linamhusu Newe kughushi nyaraka  ambaye alighushi nyaraka kwa lengo la kujipatia kiasi cha fedha cha Sh milioni 425 kwa njia  hiyo hiyo ya kughushi.

Wakili Nyantori amedai mahakamani hapo kuwa kwenye shitaka la 10 mshitakiwa Kisena na Newe walihusika kwenye utakatishaji wa fedha haramu ambapo inadaiwa kosa hilo kutendwa tarehe 16 Novemba 2015 jijini Dar es Salaam walihamisha kiasi cha 1.1 Bilioni kutoka kwenye akaunti namba 10160168505 ya Maxcom Africa Limeted kwenye benki ya Internatinal Commecial Bank kwenye kwenye akaunt ya Kisena wakijua kuwa ni zao za kughushi.

Shitaka la 11 washtakiwa wote watatu (Kisena, Kulwa na Newe) ambapo wanadaiwa tarehe 17 Novemba 2022 eneo la ilala jijini  Dar es Salaam kwenye benki ya NMB tawi la Bank House walihamisha kiasi cha shilingi kutoka kwenye akaunti ya Shirika la usafiri Dar es Salaam Dart akaunti namba 20110017710 kwenda kwenye akaunti ya Maxcom Africa Limeted wakijua kuwa ni zao la uhalifu.

Shitaka la 13 washtakiwa wote watatu wanadaiwa tarehe 19 Novemba 2015  kutakatisha kiasi cha Sh bilioni 1.1 kutoka akaunti ya Maxcom kwenda kwenye akaunti ya Kisena.

Wakili Nyantori alidai kuwa  shtaka la 14 linamkabili Kisena pekee yake ambapo anadaiwa tarehe 19 Novemba 2015 alihamisha kiasi cha 8.2 kutoka kwenye akaunti ya Maxcom kwenye kwenye akauti yake.

Shitaka hili ni sawa na lile la 16 liliofanywa na Kisena pekee yake ambapo anadaiwa tarehe 27 Novemba alihamisha kiasi cha Sh bilioni 1.1 kutoka akaunyti ya Maxcom kwenda kwenye akuati yake. Huku shitaka la 15 likiwakabili Kisena na Newe ambao wanadaiwa kutakatisha kiasi cha Sh bilioni 1.1.

Shitaka la 17 linawahusu watuhumiwa wote ambalo ni kutakatisha kiasi cha Sh milioni 425 na shitaka la mwisho ni kuisababishia hasara Dart kiasi cha Sh bilioni 4.5.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umeishakamilika  na wameomba wapewe muda kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ili hatua nyingine zinazofuata ziendelee

Washtakiwa hao, wamerudishwa rumande hadi tarehe 23 Mei, 2022 mwaka huu kesi hizo zitakapojwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

Habari Mchanganyiko

Oryx wagawa mitungi 1000 kwa viongozi wa dini, wajasiriamali Moshi

Spread the loveVIONGOZI wa dini kutoka madhehebu mbalimbali pamoja na wajasiriamali katika...

Habari Mchanganyiko

RC Geita awafunda wahitimu wapya GGML

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ametoa wito kwa...

Habari Mchanganyiko

Biteko asisitiza umuhimu wa EREA sekta ya nishati

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!