July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kisena ampa wakati mgumu Mshama jimboni

Mbunge wa Nkenge CCM, Assumpter Mshama (kushoto) akiwa na msaidizi wake wa Taasisi ya Nkenge

Mbunge wa Nkenge CCM, Assumpter Mshama (kushoto) akiwa na msaidizi wake wa Taasisi ya Nkenge

Spread the love

MBUNGE wa Nkenge CCM, Assumpta Mshama amemuomba Mkurugenzi wa Simon Group, Robert Kisena kutekeleza ahadi yake ya kusaidia Taasisi ya Nkenge Foundation Trust Fund kiasi ya sh. milioni 30 ambazo aliahidi tangu Desemba 25 mwaka jana jijini Dar es Salaam. Anaandika Dany Tibason …(endelea).

Mshama amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma ambamo vikao vya bunge la Bajeti vinaendelea.

Amesema Mkurugenzi huyo wa Simon Group aliwakilishwa na mfanyakazi wake ambaye anatambulika kwa jina moja la Charles ambapo aliahidi kuwa kampuni yao ingetoa milioni 30 kwa lengo la kusaidia upatikanaji wa vitanda vya kujifungulia kwa akina mama wajawazito kwenye hospitali za jimbo hilo.

Mbunge huyo alisema kutokana na ahadi hiyo wananchi na viongozi wa Halmashauri ya Nkenge wamekuwa wakimdai vitanda hivyo, wakati ukweli ni kuwa yeye hajapata msaada huo wa Simon Group hadi sasa.

“Kusema ukweli ahadi ya Simon Group ya kutupatia milioni 30 kwa ajili ya ununuzi wa vitanda vya wazazi kujifungua inanipa wakati mgumu kwani wenzangu kule jimboni wanaamini kuwa fedha hizo nimepewa tayari,” amesema.

Mshama alisema ombi lake ni kuhakikisha kuwa kampuni hiyo inatekeleza ahadi yake kwani cheki ambazo wamempatia zimekuwa zikionesha kuwa hakuna fedha wakipeleka bungeni.

Amesema hundi ambazo amepatiwa zipo tatu ambazo ni za mwezi Februari, Machi na Aprili mwaka huu lakini zote zimeoneka kukosa fedha hivyo kumpa wakati mgumu hivyo kukosa kutoa majibu kwa wapiga kura.

Mbunge huyo wa Nkenge amesema ni vema kampuni hiyo ikaweka bayana mbele ya vyombo vya habari kuwa imeshindwa kutekeleza ahadi yake ili imuweke yeye huru.

Amesema wananchi wa Nkenge wana imani naye kubwa kutokana na ufanisi wake kwenye kutekeleza malengo yake kwa asilimia kubwa lakini jambo dogo hilo linaweza kumchafulia sifa aliyonayo.

Hatahivyo jitihada za kumpata Kisena kupata ufafanuzi kuhusu mamalamiko hayo ziligonga ukuta baada ya kuwasiliana na Ofisa wa Simon Group hiyo Charles ambaye ndiye aliwakilisha kampuni na kumtaka mwandishi wa habari hii kuwasiliana na mkurugenzi ambaye naye simu yake iliita bila majibu.

error: Content is protected !!