July 31, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kisasi cha Uchaguzi Mkuu CCM chaanza

Spread the love

KISASI cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kushughulikia wanachama na viongozi wake wanaotuhumiwa kusaliti chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu kimeanza kutekelezwa, anaandika Christina Raphael.

Mkoani Morogoro viongozi 21 wameng’olewa madarakani kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo usaliti wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana huku 29 wakivuliwa uanachama.

Akizungumzia hatua hiyo ofisini kwake leo Rojas Romuli, Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro amesema, adhabu hiyo ni moja kati ya adhabu mbalimbali zilizotolewa kwenye kikao cha kawaida kilichofanyika tarehe 13 Machi mwaka huu ambapo Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa imepokea na kujadili tathmini ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani sambamba na kutoa adhabu kwa waliokosea.

Romuli amesema, wanachama waliokuwa viongozi wameachishwa uongozi na wengine kuachishwa uanachama na wengine kupewa onyo ni pamoja na walikuwa makatibu wa kata, Menyeviti wa CCM Kata, Wenyeviti Serikali za Vijiji, Makatibu Wenezi wa Kata na Wenyeviti wa Vitongoji.

Wengine ni wajumbe Halmashauri za Vijiji, Wajumbe Serikali za Vijiji, Mabalozi wa Shina, Wajumbe Kamati ya Siasa za Kata na wanachama wa kawaida.
Amesema kuwa, wanachama na viongozi hao walikiuka taratibu za CCM na kufanya makosa mbalimbali ikiwemo usaliti, uzembe na kutowajibika.

 

error: Content is protected !!