Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kisasi cha TRA: Gambo ahoji hatma St. Jude, Spika ataka majibu
Habari za SiasaTangulizi

Kisasi cha TRA: Gambo ahoji hatma St. Jude, Spika ataka majibu

Spread the love

 

SAKATA la Shule ya St. Jude, iliyoko jijini Arusha, kukabiliwa na ukata uliosababishwa na fedha zake kuzuiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), limetua bungeni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Sakata hilo liliibuka Desemba 2020, ambapo uongozi wa shule hiyo, ulidai TRA imezuia fedha za shule hiyo, ambazo asilimia kubwa ni za misaada kutoka kwa wafadhili wanaogharamia watoto wasiokuwa na uwezo shuleni hapo.

Leo Alhamisi tarehe 11 Februari 2021, bungeni jijini Dodoma, Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo ameuliza suala hilo akitaka kujua, nini kinaendelea ili kuiwezesha shule hiyo kuendelea kutoa elimu kwa ufanisi.

“Mkoani Arusha kuna shule inaitwa St. Jude, inasomesha watoto wenye mazingira magumu na kupitia misaada ya watu mbalimbali huko duniani.

Mrisho Gambo, Mbunge wa Arusha Mjini (CCM)

“Hapa karibuni, TRA imeenda kwenye akaunti ya shule hiyo imechukua fedha na kusababisha shule hiyo kupata misukomsiuko na kufungwa. Serikali ina mpango gani kutoa ahueni kwa shule hii?” amehoji Gambo.

Gambo ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kabla ya ubunge amesema, kufungwa kwa shule hiyo kumesababisha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu mkoani humo, kukosa masomo.

Akijibu swali hilo, Omary Kipanga ambaye ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema, suala hilo atalifanyia kazi, kisha atatoa majibu litakapopatiwa ufumbuzi wake.

“Kama alivyobainsiha uwepo wa shule hiyo na changamoto zilizotokea na wenzetu wa TRA, mheshimiwa spika, naomba suala hili tulichukue, twende tukalifanyie kazi na baadaye tutaweza kutoa majibu muafaka kwa mbunge na Mkoa wa Arusha kiujumla,” amesema Kipanga

Baada ya majibu hayo, Spika wa Bunge, Job Ndugai alimsisitiza Naibu Waziri huyo, akimuagiza ampe nakala ya majibu ya serikali kuhusu sakata hilo.

“Hiyo ni ahadi ambayo mheshimiwa naibu waziri tutaomba itekelezwe na ningenda kupata nakala ya majibu hayo yatakapokuwa tayari. Sababu ni hatima ya watoto wa masikini kwa hiyo, tungependa kujua hatima ya jambo hilo ili tujiridhishe,” amesema Spika Ndugai.

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai

Tarehe 1 Desemba 2020, baadhi ya wazazi wa watoto wanaosoma shule hiyo ya mchepuo wa kiingereza, waliandamana hado Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, wakilalamikia uamuzi wa TRA kufungia kaunti za shule hiyo, hali iliyosababisha kusitishwa kwa masomo.

Uaongozi wa shule hiyo, uliamua kusitisha masomo baada ya kushindwa kuhimili gharama za kuendesha shule baada ya TRA kuzifunga akaunti za shule kwa madai kwamba, inadai kodi ya muda mrefu.

Shule hiyo, ilikataa kulipa kodi hiyo kwa madai kwamba, haifanyi biashara kwani, fedha inazopokea kutoka kwa wafadhili, zinagharamia kuwasomesha watoto wa masikini ambao ufadhili wake ni wa asilimia 100.

MwanaHALISI Online imeutafuta uongozi wa Shule ya St. Jude kwa simu ili kujua kama imemaliza tofauti zake na TRA, ambapo umesema hauko tayari kuzungumzia suala hilo.

Hata hivyo, umesema shule hiyo haijafungwa, bali inaendelea kufundisha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!