May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kisa utovu wa Nidhamu, Mkude kufanyiwa vipimo

Jonas Mkude

Spread the love

 

KAMATI ya nidhamu ya klabu ya Simba, iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake Seleman Kova, imeuagiza uongozi wa klabu hiyo, kumfanyia vipimo vya afya kiungo wake Jonas Mkude, kabla ya kutoa hukumu mara baada ya kukabiliwa na makossa ya utovu wa nidhamu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Kamati hiyo ambayo ilkutana tarehe 5 juni kusikiliza shauli la mchezaji huyo, ambaye hakuripoti kambini na kutonekana mazoezini tarehe 18 Mei, 2021 imeamua kuahilisha hukumu hiyo ambayo ilipaswa kutolewa leo tarehe 7 Juni, 2021 na kutoa mapendekezo hayo.

Katika taarifa ya kamati hiyo, pamoja na mambo yote imetoa mapendekezo kwa menejiment ya klabu hiyo, kutaka mchezaji huyo kupelekwa kwenye hospital ya Taifa ya Muhimbili, kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya vya Afya, ili kupata taarifa ya kitabibu, kutokana na mchezaji huyo kufanya makossa yanayojirudia.

Kamati hiyo imetoa mapendekezo hayo, mara baada ya kubaini kuwa makossa yanayomkabili Mkude huwa ni ya kujirudia, licha ya kutiwa hatiani na kupewa adhabu mbalimbali.

Kwenye kesi hiyo mchezaji Jonas Mkude aliwakilishwa na Wakili Jonas Mfinanga, huku upande wa klabu ya Simba, uliwakilishwa na Wakili Michael Mhina.

Hii ni mara ya pili kwa Mkude kusimamishwa ndani ya klabu ya Simba, kwa makosa ya kinidhamu katika siku za hivi karibuni licha ya kuomba radhi.

Mara ya kwanza Mkude alisimamishwa ilikuwa tarehe 28 Desemba, 2020 ambapo uongozi wa klabu hiyo ulisema kuwa, umemsimamisha kutokana na masuala ya utovu wa nidhamu pamoja na masuala mengine.

Kamanda mstaafu na Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu klabu ya Simba Suleiman Kova

Uongozi wa klabu hiyo ulifikia hatua hiyo, ili kamati ya nidhamu ifanye uchunguzi juu ya tuhuma zimamkabili kiungo huyo.

error: Content is protected !!