KLABU ya Yanga imeonekana kusikitishwa na kitendo cha Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kumchagua Ahmed Arajiga kuwa mwamuzi wa mchezo wao wa fainali dhidi ya Simba kwa madai ya kuwa refa huyo kuchezesha michezo mitatu mfululizo ya wapinzani wao. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Kigoma … (endelea).
Mchezo huo wa fainali utapigwa siku ya Jumapili Julai 25, Mwaka huu, kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, mjini Kigoma.
Yanga wametoa malalamiko yao ikiwa siku moja tu toka, Shirikisho hilo kuweka hadharani majina ya waamuzi katika mchezo huo wa fainali.
Katika taarifa yao, Yanga wanaamini kuwa Tanzania kuna waamuzi wengi, wenye uwezo hivyo kitendo cha kumrudia mwamuzi moja katika michezo mitatu ya Simba inatia shaka.
Mwamuzi huyo ndiye aliyechezesha mchezo wa hatua ya robo fainali wa kombe hilo, kati ya Simba na Dodoma Jiji na kisha kuchezesha mchezo wa nusu fainali kati ya Simba na Azam Fc ambao ulimalizika kwa Simba kutoka na ushindi wa bao 1-0.
Aidha uongozi wa Yanga umeitaka TFF na kamati ya mashindano kutafakari juu ya maamuzi waliyofanya.
Waamuzi wengine waliopangwa kwenye mchezo huo, ni Frednand Chacha ambaye ni mwamuzi msaidizi namba moja kutoka Mwanza, Mohamed Mkono mwamuzi namba mbili kutooka Tanga, huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Elly Sasii kutoka Dar es Salaam.
Leave a comment