Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Kisa mauaji: Dk. Mpango ampa siku saba IGP, ‘tumechoka’
Habari Mchanganyiko

Kisa mauaji: Dk. Mpango ampa siku saba IGP, ‘tumechoka’

IGP Simon Sirro
Spread the love

 

MAKAMU wa Rais, Dk. Philip Mpango ametoa siku saba kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini – IGP Simon Sirro kuwakamata watuhumiwa wa matukio ya mauaji pamoja na kukomesha matukio hayo nchini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Dk. Mpango ametoa agizo hilo leo tarehe 26 Januari, 2022 alipotembelea wafiwa wa ndugu wa marehemu watano wa familia moja waliofungiwa ndani na kuuawa.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika kijiji cha Zanka wilayani Bahi Mkoani Dodoma.

Aidha, Dk. Mpango ametoa maelekezo kwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama mkoani Dodoma kuhakikisha vinafanyia kazi suala hilo la mauaji na kuwasilisha taarifa yao ndani ya siku saba kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza wakati wa kuwafariji wafiwa hao Dk. Mpango ameshangazwa kutokea kwa mauaji hayo na marehemu kukaa siku tatu na kuharibia ndani bila majirani wala uongozi wa kijiji kutokuwa na taarifa.

“Nimefika hapa kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan kuja kutoa pole kwa familia ambayo imetendewa ukatili huu, lakini kutoa pole kwa kijiji cha Zanka na vijiji vyote vya jirani… poleni sana.

“Kwa kweli mheshimiwa Rais amesononeka sana na tukio hili ni la kikatili na la kinyama. Lakini bado tuna maswali mengi maana wazee hawa baba na mama itachukua miaka mingi machozi yao kukauka huku kukiwa na maswali mengi,” amesema.

Makamu wa Rais, Dk. Phillip Mpango

Aidha, ametoa wito kwa familia zote katika kata hiyo ya Zanka na nchi nzima kujuliana hali.

“Watanzania tuna sifa duniani ya kupendana, inakuwaje mwanafamilia haonekani siku tatu na wanafamilia wapo karibu, hata hodi nyumba hii, kuna tatizo kubwa, majirani mpo kimya kabisa…yaanio hata kushtuka mbona jirani haonekani!

“Kuna shida, uongozi wa mtaa, nyumba kumi, kijiji kimya kabisa mpaka mwili wa binadamu unaharibika ndio tunashtuka kweli? Alihoji Dk. Mpango.

Amewasihi wananchi wa kijiji hicho na Watanzania kwa ujumla kupendana na kujuliana hali.

“Pale penye matatizo hata kimila tukae tuzungumze, kama wakatili wauaji hawa wanatoka vijiji jirani utaratibu wetu mgeni anapoingia kijijini anatolewa taarifa kwa uongozi,” amesema.

Aidha, amemuagiza Mkuu wa wilaya hiyo, kurudi eneo hilo na kuzungumza na wanakijiji kuhusu ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao.

“Ulinzi huu unaanza na sisi wenyewe ukiona jambo halieleweki unatolea taarifa mapema siyo kusubiri kuja kulia namna hii.

“Nawataka viongozi kuanzia ngazi ya ubalozi kuanzia sasa tufuatlie maisha ya wananchi wetu,” amesema

Pia amewaomba viongozi wa dini wasaidie kuzungumza na wananchi kwenye nyumba zao za ibada kuwakumbusha kwamba hakuna binadamu mwenye haki ya kuondoa uhai wa mtu mwingine.

“Kama una matatizo na jirani na ndugu yako zipo njia… wapo wazee, Serikali ipo, kwa hiyo viongozi wa dini naomba sana mkatukumbushe wajibu wetu kwa Mungu na kwa binadamu wenzetu, hata simba hawauani, sasa sisi tumegeuka wa hovyo kuliko wanyama,” amesema na kuongeza;

“Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Dodoma, nifikishie salam kwa IGP, mauaji haya nchi nzima yakome, mfanye kazi ya kuyazuia, polisi mna kazi kubwa ya kufanya nchini. Rais Samia na mimi tumechoka hatuwezi kuongoza nchi yenye mauaji namna hii,” amesema.

Ameitaka Idara ya Upelelezi ya mkoa wa Dodoma ihakikishe saa 24 inafanya kazi watuhumiwa wa mauaji hayo wanapatikana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!