June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kisa Mahari kubwa, Baba aua kijana wake baada ya kung’ang’ania kumuoa mchumba’ke

Kamanda wa Polisi mkoani Singida, Stella Mutabihirwa

Spread the love

 

KIJANA aliyefahamika kwa jina Nchimwa Magidu Ndula (22), amuawa kwa kipigo kutoka kwa baba yake mzazi, Magidu Ndula Jisusi (55) baada ya kumtorosha binti ambaye alikuwa anatarajia kumuoa na kumpeleka nyumbani kwao kama mke.  Anaripoti Victoria Mwakisimba, TUDARCo … (endelea).

Tukio hili lilitokea tarehe 8 Oktoba, 2021 huko mkoani Singida katika kitongoji cha Madalawa kijiji cha Mlandala kata ya Urughu wilayani Iramba.

Chanzo kikubwa cha mauaji hayo kinadaiwa kwamba ni kitendo cha kijana huyo kujichagulia mchumba katika sherehe za jamii ya kisukuma kwa taratibu za kabila hilo zinazojulikana kama “chagulaga”.

Kitendo hicho hakikuafikiwa na baba mzazi wa kijana huyo kwa sababu alidaiwa mahari kubwa na alipomwambia kijana wake kumrudisha binti huyo aligoma kabisa.

Kwa mujibu wa mashuhuda, ndipo baba huyo akaamua kumwadhibu mwanae kwa viboko hali iliyopelekea umauti wa kijana huyo.

Kamanda wa Polisi mkoani Singida, Stella Mutabihirwa  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi unaonyesha marehemu alifikwa na umauti baada ya kupigwa sana na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kamanda Stella amesema jeshi la polisi linamshikilia mzee Jisusi kwa mahojiano zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani ambako atajibu mashtaka yanayo mkabili.

error: Content is protected !!