Sunday , 29 January 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Kisa kugomea chanjo ya Corona; watabibu 3,000 watimuliwa, waanzisha mgomo wa kutokula
Kimataifa

Kisa kugomea chanjo ya Corona; watabibu 3,000 watimuliwa, waanzisha mgomo wa kutokula

Spread the love

 

SERIKALI ya Ufaransa imetangaza kuwaachisha kazi wahudumu wa afya 3,000 waliogoma kuchanjwa chanjo ya Corona licha ya nchi hiyo kupitisha sheria ya lazima kwa wahudumu wa sekta hiyo kuchanjwa. Anaripoti Helena Mkonyi TUDARCo kwa msaada wa vyombo vya habari vya kimataifa … (endelea).

Pia mmoja wa watatibu hao Thierry Paysant ametangaza mgomo wa njaa yaani kutokula hadi hapo Serikali itakapowarejesha kazini.

Paysant ambaye alikuwa mhudumu wa kitengo cha udhibiti moto katika hospitali ya Nice nchini humo, aliandamana mitaani huku akiwa na bango lililoandikwa ‘mgomo wa njaa’ na kusisitiza kuwa mbali na hatua hiyo watachukua hatua zaidi kuishinikiza serikali.

Paysant amesema hakuwa na nia ya kwenda kinyume na matakwa ya taratibu za chanjo lakini kitendo cha serikali kuwatimua wafanyakazi wenzie kisha kushindwa kuchanja kabla ya  tarehe ya mwisho kuchanja ndicho kilichomkera.

“Nina huzuni  ambayo haielezeki kwa sababu chanjo yenye imeletwa kwa vurugu na kuanza kutulazimisha wakati hii inapaswa kuwa hiyari,” amesema.

Aidha, Waziri wa Afya nchini humo, Olivier Veran ametangaza kuwa tarehe ya mwisho wa kuchanja ilikuwa jana tarehe 15 Septemba, 2021 ndio maana leo Serikali imechukua hatua ya kuwatimua wafanyakazi hao.

Amesema Serikali imeamua kuchukua uamuzi huo ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.

Kwa mujibu wa mtandao wa takwimu za kila muda duiani ‘Worldometer’, hadi kufikia tarehe 16 Septemba Ufaransa ilikuwa na maambukizi ya Corona milioni 6.9 huku kukiwa na vifo 115,829.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

DCI ajitosa uchunguzi matokeo uchaguzi mkuu Kenya

Spread the loveOFISI ya Mkurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Kimataifa

Uganda yaanza kuchimba mafuta

Spread the love  UCHIMBAJI wa kwanza wa mafuta kibiashara nchini Uganda umeanza...

Kimataifa

Afrika kusini waandamana kushinikiza serikali kumaliza tatizo la umeme

Spread the love  MAMIA ya wafuasi wa Chama cha upinzani nchini Afrika...

error: Content is protected !!