RAIS wa Shirikisho la Soka nchini Algeria (FAF) Charafeddine Amara pamoja na bodi nzima ya shirikisho hilo, amejiuzulu baada ya timu ya Taifa hilo kushindwa kutinga katika mashindano ya Fainali za Kombe la Duania yanayotarajiwa kupigwa huko nchini Qatar Novemba mwaka huu.
Amara mwenye umri wa miaka 56 amechukua uamuzi huo tarehe 31 Machi, 2022 baada ya Algeria kufurumushwa na ‘Simba asiyefugika’ – Cameroon.
Jumanne wiki hii Cameroon waliwachapa ‘Mbweha hao’ wa Jangwani, Algeria bao 2 – 0 mtanange uliopigwa katika uwanja wa Mustapha Tchaker mjini Blida nchini Cameroon.
Aidha, akizungumza na waandishi wa habari siku mbili baada ya kadhia hiyo, Amara alitangaza kujiuzulu.

Hata hivyo, Rais huyo alimuomba Kocha Mkuu wa Algeria Djamel Belmadi (46) aliyejuzulu kurejea katika kibarua chake.
“Nimeamua kujiuzulu sio kwa sababu ni sehemu ya majukumu yangu, hapana… hii ni sehemu ya wajibu wangu kisheria.
“Nimepokea simu nyingi zinazonipa wakati mgumu baada ya mtu nisiyemfahamu kuweka namba yangu ya simu kwenye mitandao ya kijamii, kwa hiyo tumekubaliana na mabadiliko haya,” alisema.
Inaelezwa kuwa tangu mwaka 1992 hakuna Rais wa Shirikisho hilo la Algeria aliyewahi kudumu madarakani hadi muda wake kukamilika.
Leave a comment