January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kisa Corona wachezaji wanne Morocco kuikosa Ghana AFCON

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Morocco

Spread the love

 

Wachezaji wanne wa timu ya Taifa ya Morocco wataukosa mchezo wa leo dhidi ya timu ya Taifa ya Ghana, kwenye michuano ya kombe la mataifa Afrika ‘AFCON’ kufuatia kukutwa na maambukizi ya virusi vya Uviko 19. Anaripoti mwandishi Wetu…(endelea)

Mchezo huo wa kundi C utapigwa majira ya saa 1 kamili usiku kwenye dimba la Stade Ahmadou Ahidjo, jijini Yaounde.

Taarifa ya kukosekana kwa wachezaji hao ilithibitishwa jana na kocha mkuu wa Morocco Vahid Halilhodžić kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Wachezaji hao watakaokosa mchezo huo ni washambuliaji Strikers Ryan Mmaee, Youssef En-Nesyri, Ayoub El Kaabi sambamba na kiungo wao Aymen Barkok.

Kwa upande wa timu ya Taifa ya Ghana hakuna kisa chochote kilichoripotiwa ambacho kinaweza kusababisha baadhi ya wachezaji kukosa mchezo huo.

error: Content is protected !!