October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kisa corona: Makonda atangaza siku ya shangwe Dar

Paul Makonda

Spread the love

PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania, amewaagiza wananchi wa jiji hilo kurejea kwenye shughuli zao kama ilivyokuwa awali. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Makonda amesema hayo leo Jumanne tarehe 19 Mei, 2020 alipotembelea ujenzi wa Daraja la Tanzanite maarufu kama daraja la Coco beach.

Amesema licha ya Rais wa Tanzania, John Magufuli kutoa siku tatu za shukrani kuanzi Ijumaa hadi Jumapili yeye ameongezea siku ya Jumapili itakuwa siku ya shangwe.

“Tunawaomba wenye hotel, bar wenye kampuni wenye biashara zote turudi kazi ilimradi unajua kunawa kwa maji yanayotiririka kwa sabuni, unajua kuwa na ‘social distance’ maana yake kukaa umbali unaotakiwa lakini la mwisho huna sababu za kukaa kwenye msongamano,” amesema Makonda

“Dk Magufuli ametupa siku tatu za shukrani  tumshukuru mungu wetu maana yake ijumaa , jumamosi na jumapili lakini mimi naomba niongezee ikifika jumapili kila mmoja apige vigelegele na kila aina ya fujo unayoijua ikiwa ni ishara kuwa mungu wetu ametushindia,” amesema Makonda.

Wakati huo huo, Makonda amewataka wananchi waliondoka jijini kwa ajili ya kukimbia Corona.

“Natoa wito kwa wananchi wote waliondoka mikoani kwa ajili ya kusubiri Corona ipite warudi watatukuta tunaafya njema na tunaendelea kufanya kazi… mauti huikimbii tarehe ikifika imefika tu,” amesema.

error: Content is protected !!