JANGA la ungonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19), unaoendelea kushika kasi nchini India, umesababisha Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), kusitisha safari zake kati ya Dar es Salaam-Tanzania kwenda nchini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Hadi leo asubuhi Jumatano, tarehe 5 Mei 2021, maambukizi ya corona nchini India, yamefikia milioni 20.66, ikiwa nchi ya pili kwa maambukizi dunia, ikitanguliwa na Marekani yenye maambukizi milioni 33.27.
Kati ya maambukizi milioni 20.66 ya India, waliofariki dunia wakiwa 226,188 na waliopona ugonjwa huo wakiwa milioni 16.95.
Kutokana na janga hilo, jana Jumanne, tarehe 4 Mei 2021, Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi alitangaza kusitishwa kwa safari za ndege kwenda India.
Alisema, abiria wote wenye tiketi za ATCL, wanashauriwa kuwasiliana na ofisi za ATCL au mawakala wao kwa taratibu za kubadilisha tiketi ili zitumike pindi safari zitakaporejeshwa tena bila gharama yoyote.
Leave a comment