October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kisa bintiye kunyolewa nywele… mzazi adai fidia ya Sh bilioni 2.3

Spread the love

 

BABA mmoja raia wa Marekani amedai alipwe dola milioni moja sawa na Sh bilioni 2.3 baada ya binti yake mwenye umri wa miaka saba kunyolewa nywele na mwalimu wake. Anaripoti Noela Shilla TUDARCo … (endelea).

Jimmy Hoffmeye ameishtaki shule anayosoma mtoto wake pamoja na wafanyakazi wake wawili kwa kumnyoa binti yake bila ruhusa ya mzazi.

Kwa mujibu wa mashtaka yake, Hoffmeyer amesema haki ya mtoto wake ya kuwa na nywele ilikiukwa na ameamua kumhamisha mtoto wake katika shule hiyo.

Uchunguzi uliofanywa kuhusiana na kisa hicho, ulibaini kuwa licha ya kumnyoa nywele, mwalimu huyo pia alimbagua kwa misingi ya rangi yake.

Mwalimu huyo alipatikana na hatia lakini aliendelea kufanya kazi katika shule ya Ganiard iliyopo Michigan.

Mashtaka dhidi ya shule na wafanyakazi wake wawili kumhusi bintiye yalipelekewa katika Mahakama ya Michigan nchini humo.

error: Content is protected !!