KIRUSI kipya cha Corona kilichopewa jina la ‘Mu’ au B.1.621 kimeanza kutikisa nchi kadhaa za Bara la Amerika kusini na Ulaya huku kikidaiwa kuwa kinaweza kukwepa chanjo ya Corona. Anaripoti mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
WHO ilisema kirusi hicho kina mabadiliko yanayoonesha hatari ya kuishinda nguvu ya chanjo na kwamba utafiti zaidi unahitajika kukielewa.
Hayo yamebainishwa tarehe 30 Agosti mwaka huu na Shirika la Afya Duniani (WHO) kupitia jarida lake baada ya Shirika hilo kukingiza kirusi hicho katika orodha ya virusi hatari vya Corona.
Kirusi hicho ambacho kilianza kugunduliwa huko nchini Colombia, hadi sasa kimeathiri nchi 389 kati bara la Amerika Kusini, Kaskazini na Ulaya.
Kwa mujibu wa Ofisa wa afya nchini Colombia, Marcela Mercado amesema kirusi MU ndicho kinachosambaa zaidi nchini humo na kinahusika na wimbi baya zaidi la janga la corona.
Mercado ameiambia redio moja nchini humo kwamba kirusi cha “Mu” kinahusika na wimbi kali la tatu la maambukizi kati ya April na Juni mwaka huu.
Nchi hiyo ambayo imekuwa ikirekodi vifo 700 kila siku vitokanavyo na Corona, karibu theluthi mbili ya vipimo vilivyofanywa kutoka kwa watu waliofariki vilionesha waliambukizwa kirusi cha Mu.
Leave a comment