January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kipindupindu chazidi kuwa tishio Dar

Spread the love

UGONJWA wa kipindupindu wazidi kuwa tishio Jijini Dar es Salaam hadi kufikia leo kuna jumla ya wagojwa 4076 na vifo 53 katika Wilaya zote tatu. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Katika Wilaya ya Kinondoni walipatikana wagonjwa 1963 na vifo 18, Temeke wagojwa 621 na vifo 14, na Ilala wagojwa 1492 na vifo vipatavyo 21.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam wakati wa semina fupi ya waandishi wa habari iliyofanyika katika ukumbi wa New Afrika, Mratibu wa huduma za afya ya jamii Victoria Bura amesema, wagonjwa hao walilazwa katika kambi maalumu za kutibu ugojwa huu zilizopo Vijibweni, Buguruni na Mburahati.

Bura amesema, licha ya ugonjwa huo kuingia kwa kasi jijini, Wizara ya afya imefanikiwa kuudhibiti kwa kiasi kikubwa huku wakishirikiana na Taasisi nyingine zilizojitolea kutoa misaada mbalimbali.

“Kutokana na jitihada mbalimbali zilizotumika kudhibiti ugonjwa huu katika baadhi ya kambi wagojwa wamepungua kama Wilaya ya Kinondoni siku ya jana hakuna mgonjwa aliyepelekwa. Jitihada za kutoa elimu, maji safi yenye dawa pamoja na dawa vimesaidia kuwapunguza wagojwa kambini.

Naye mkuu wa Kitengo cha dharura na maafa Mkoa Merry Kitambi amesema kuwa, mlipuko wa ugonjwa huo Dar es Salaam ulianza Agosti 15 mwaka huu na sasa umesambaa katika mikoa 17.

Amesema, kutokana na takwimu za nchi nzima hadi sasa kuna wagonjwa 7598 na vifo 102, katika mikoa 17 na vijiji 39.

“Sekta ya afya kitengo cha dharura kinahitaji sana ushirikiano wa sekta nyingine kwa kuwa inaelemewa sana. Ndio maana leo tumeamua kukutana na wanahabari ili watusaidie kutoa elimu mitaani jinsi ya kujikinga na ugonjwa huu”. amesema Kitambi.

Aidha, semina hiyo ya siku moja imeandaliwa na Wizara ya afya kwa udhamini wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa jamii na njia ya kutoa mafunzo ya kujikinga na ugonjwa huo ili kuutokomeza kabisa.

error: Content is protected !!