JUMLA ya watu 13491 wameathiri na ugonjwa wa kipindupindu na kati yao,watu 205 wafariki dunia kutokana na ugonjwa wa kipindi cha miezi sita. Anaandika Regina Mkonda … (endelea).
Naibu Waziri wa Afya Dk. Hamisi Kigwangalla amesema katika kipindi cha wiki iliyoanza ya tarehe 4 hadi 10 mwaka huu jumla ya wagonjwa 615 wameripotiwa sehemu mbalimbali nchini na wagonjwa 3 kufariki dunia kutokana na kukumbwa na ugonjwa huo.
Aidha ameitaja mkoa ambayo bado inasumbuliwa na ugonjwa huo ni pamoja na Morogoro, Simiyu, Singida, Pwani, Geita, Tanga, Arusha, Manyara, Mara na Mwanza.
Amebainisha kuwa miongoni mwa maeneno ambayo yanatajwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi ya wagonjwa wapya wa kipindupindu ni Manispaa ya Morogoro wagonjwa 87, halimashauri ya Morogoro 66, Arusha 50, Singinda wilaya ya Iramba 40 na manispaa ya Dodoma 33.
Pia ameitaja mikoa ambayo mpaka sasa haina maambukizo mapya ya ugonjwa huo kuwa ni Mtwara, Katavi, Mbeya, Rukwa, Kagera, Lindi na kigoma.
Amewataka wananchi ambao hawajapata maambukizi ya ugonjwa huo kuendelea kuchukua taadhari kwa kunywa maji safi na salama, kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira safi, kuosha matunda na kunawa mikono kabla na baada ya kula.
More Stories
Rais Samia ataka wanaume waone wake zao wanavyojifungua
Jengo la mama na mtoto CCBRT kuhudumia wajawazito 12,000 kwa mwaka
Mkakati CCBRT wapunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 47