October 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kipigo Stars. Kocha alia na Refa

Spread the love

MARA baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Benin kwa bao 1-0, kocha wa kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen ameonekana kutofurahishwa na baadhi wa mwamuzi wa mchezo huo, kufuatia wapinzani wake kucheza rafu nyingi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa kufuzu fainali za kombe la Dunia nchini Qatar 2022, ulipigwa jana majira ya saa 10 jioni kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Poulsena amesema kuwa, wakati wa mchezo huo wachezaji wa Timu ya Taifa ya Benin walikuwa wakicheza rafu nyingi kwa kuwagonga miguu kwa nyuma wachezaji wa Taifa Stars na mwamuzi hakuchukua hatua yoyote.

“Kitu nisichokipenda kwenye mchezo wa leo ni jinsi mwamuzi alivyokuwa anawaacha wachezaji wa Benin kucheza rafu kwa nyuma, na ukifanya kosa hilo unapaswa kuadhibiwa na Benin wamefanya hivyo zaidi ya mara nne.” Alisema Kocha huyo

Kim Poulsen, kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania

Aidha Poulsen aliendelea kusema kuwa alimfuata mwamuzi huyo Alvaco Ceelso Kutokea nchini Msumbiji mara baada ya mchezo kumalizika na kumueleza asivyokubaliana na maamuzi yake, huku akisisitiza hamtupii lawama refa kwa kuwa ajashinda mchezo huo.

“Nilimwambia mwamuzi baada ya mchezo kuisha kwamba ulikuwa unakosea na siwezi kumuongelea refa kwa kuwa sijashinda ilikuwa tujiangalie wenyewe kutumia zile nafasi na tutajiandaa vizuri kwa mchezo wa marudiano ikiwa tuna siku mbili tu.” Aliongezea kocha huyo

Katika hatua nyingine Poulsen anaamini bado wachezaji wake wananafasi ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa marudiano nchini Benin utakaopigwa Oktoba 10, 2021

“Bado ninaamini wachezaji wangu pamoja na timu yangu kwamba watafanya kweli nchini Benin ili tuweze kupata matokeo na kwa jinsi tulivyocheza leo nadhani wenyewe wameona” Alisema kocha huyo

Kwa matokeo hayo ya jana Stars imeshuka mpaka nafasi ya tatu ikiwa na alama nne baada ya kucheza michezo mitatu, huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Jamhuri ya Congo wenye pointi tano, mara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Madascar huku Benin akiongoza kundi akiwa na pointi saba.

Bao pekee la Benin kwenye mchezo wa jana lilifungwa na Steve Mounie kwenye dakika ya 71.

 

 

 

 

error: Content is protected !!