May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kipa Simba afiwa na Mama Yake

Spread the love

Mlinda mlango namba mbili wa klabu ya Simba Beno Kakolanya, amepata pigo la kufiwa na Mama yake mzazi Eva Mwankusye leo asubuhi Jijini Mbeya. Anaripoti Damas Ndelema/TUDARCo

Kakolanya amepata pigo hilo, akiwa nchini Morocco ambapo kikosi cha klabu ya Simba kimeweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2021/22.

Taarifa ya kifo cha Mama mzazi wa mchezaji huyo imetolewa kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii Instagram wa klabu ya Simba na kumruhusu mchezaji huyo kurejea nchini kwa ajili ya mazishi ya Mama yake mzazi.

Taarifa kamili ya klabu ya Simba ilieleza hivi “Uongozi wa Klabu ya Simba, umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa mama mzazi wa mlinda mlango wetu Beno Kakolanya,Eva Mwankusye uliotokea leo asubuhi mkoani Mbeya.”

“Kutokana na msiba huo, Simba SC imempa Kakolanya ruhusa ya kurejea nchini kwa ajili ya kushiriki katika msiba huo.”

“Simba inaungana na familia ya Beno kwenye msiba huu mzito, tunamuomba Mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.”

“Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.” ilieleza taarifa hiyo

error: Content is protected !!