May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kiongozi Yanga amkataa Ajibu

Ibrahim Ajibu, mshambuliaji wa Yanga

Spread the love

 

Mara baada ya kuwepo kwa fununu nyingi ya mshambuliaji wa klabu ya Simba Ibrahim Ajibu kutaka kusaini Yanga, Arafati Haji ambaye ni mmoja ya mjumbe wa kamati tendaji ya klabu hiyo amefunguka kuwa mchezaji huyo hawezi kusaini Yanga. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Maneno ya kiongozi huyo yamekuja kufuatia andiko lililowekwa na mmoja ya mchambuzi wa maswala ya mpira kwenye mtandao wa Twiiter na kuonesha faida ambayo Yanga watapata ndani ya Uwanja kama wakimrejesha mchezaji huyo.

Katika kujibu taarifa hiyo kiongozi huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Fedha ndani ya klabu hiyo aliona kama mchambuzi huyo anampigia debe ajibu kurejea Yanga na kumwambia kuwa wamtafutie timu nyingine na Yanga aliyokuwepo yeye haiwezi kumsajili.

Ajibu kwa sasa anamaliza mkataba wake ndani ya Simba mara baada ya msimu huu kukamilika na anahusishwa na tetesi nyingi za za kurejea kwenye klabu yake ya awali ya Yanga ambayo aliitumikia kwa miaka miwili.

Arafat Haji, Mjumbe wa kamati ya utendaji Yanga

Toka amerejea ndani ya kikosi cha Simba mchezaji huyo ameonekana kutopata nafasi ya kucheza mara kwa mara kutokana na kikosi hiko kusheheni wachezaji hodari katika kila idara.

error: Content is protected !!