January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kiongozi wa vijana wa JKT atekwa

Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefua, ni mmoja wa viongozi waliokutana na vijana hao waliohitimu mafunzo ya JKT

Spread the love

GEOGE Mgoba, kongozi wa vijana waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), waliokuwa wakishinikiza serikali ya kutekeleza ahadi yao ya kupatia ajira ametekwa.

Taarifa zinasema, Geoge ametekwa na wanaodaiwa kuwa watu kutoka Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).

Mgomba ni miongoni mwa vijana waliokutana na viongozi wa juu wa serikali, akiwemo Balozi Ombeni Sefue.

Serikali iliahidi ulimwengu kuwa vijana wote watakaomaliza JKT watapa ajira. Ahadi hiyo haijatekelezwa.

Kutekwa kwa George kumefanywa kwa malengo mawili: Kwanza, kumshawishi alegeze msimamo wa kuwaunganisha wenzake wanaoshinikiza serikali kutekeleza ahadi yake hiyo mara moja.

“Lakini ikiwa hilo litashindikana, basi mpango umeandaliwa wa kummaliza katika staili ileile iliyofanywa kwa Dk. Steven Ulimboka,” anaeleza mmoja wa viongozi walioko katika mradi huo.

Kwa mujibu wa mtandao wa MwanaHALISI Forum, Geoger ametekwa ili kutimiza mpango wa serikali wa kuzuia wimbi la vijana waliomaliza mafunzo ya JKT, kuisumbua serikali.

“Tunawafahamu waliomteka Geoger. Nitawaumbua muda si mrefu, humuhumu MF,” anaeleza mtoa taarifa wa MwanaHALISI Online.

Anasema aliyemteka Geoger, siyo Ramadhan Ighondo ambaye alitajwa katika sakata la kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka.

“Hawa ni tofauti,” anasema na kuongeza, “Ninamjua na tutawaumbua muda si mrefu.

error: Content is protected !!