March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kiongozi wa Bavicha anusurika kifo katika ajali

Gari la Edward Simbeye baada ya kupata ajali

Spread the love

EDWARD Simbeye, Katibu Mwenezi wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), amepata ajali ya gari, anaandika Hamisi Mguta.

Ajali hiyo imetokea wakati Simbeye akiwa safarini akitokea Dar es Salaam kwenda Moshi, Kilimanjaro.

Simbeye amesema sababu ya ajali ni kufyatuka tairi la mbele kushoto kusababisha gari kupoteza mwelekeo na kuanguka kando mwa barabara eneo la Kawawa mjini Moshi.

“Tunamshukuru Mungu tumemetoka salama, mimi pamoja na mdogo wangu. Tulikuwa tunaenda nyumbani kwa sababu za kifamilia,” amesema Simbeye.

error: Content is protected !!