Saturday , 30 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Kiongozi upinzani Senegali agoma kula, alazwa
Kimataifa

Kiongozi upinzani Senegali agoma kula, alazwa

Spread the love

MWANZILISHI wa Chama cha Siasa cha PASTEF nchini Senegal, Ousmane Sonko amelazwa katika Hospitali Kuu katika mji mkuu wa Senegal, Dakar baada ya kuwa kwenye mgomo wa kula chakula akiwa gerezani. Anaripoti Isaya Temu, TUDARCo…(endelea)

Sonko (49), alikamatwa tarehe 28 Julai 2023 na ameshtakiwa kwa kupanga uasi, kudhoofisha usalama wa serikali na ushirika wa uhalifu na kundi la kigaidi na alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa makosa hayo.

Kiongozi huyo wa upinzani nchini Senegal ambaye amekuwa kwenye mgomo wa kula siku mbili zilizopita akipinga kuzuiliwa kwake amelazwa hospitalini, wameeleza  na wafuasi wake wa Chama cha PASTEF.

PASTEF kimesema Sonko amelazwa kwa huduma ya dharura na mamlaka inawajibika kwa hali yake.

“Kabla ya kufungwa kwake, alikuwa na afya njema na hakuwa na magonjwa yanayojulikana,” kilisema.

Cire Cledor Ly, mmoja wa mawakili wa Sonko alithibitisha kulazwa hospitalini kwenye shirika la habari la AFP lakini hakuzungumzia hali yake.

Kukamatwa kwake na kuvunjwa kwa chama chake kulizua maandamano mabaya mjini Dakar wiki iliyopita.

Watu wawili wanadaiwa kupoteza maisha wakati wa machafuko hayo, huku wengine kadhaa wakijeruhiwa.

Hatua hizo pia zilijiri wiki chache baada ya hakimu kumpata na hatia Sonko, katika kesi tofauti ya kushawishi vijana na kumhukumu kifungo cha miaka miwili jela. Hukumu hiyo ilizua mapigano yaliyosababisha vifo vya watu 16 kwa mujibu wa serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wadukuzi wa Kichana waiba barua pepe 60,000 za Serikali ya Marekani

Spread the loveWADUKUZI wa kichana wamedukua barua pepe 60000 serikali ya Marekani...

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

Kimataifa

Kampuni ya mali ya China Oceanwide yapata agizo la kufilisiwa huko Bermuda

Spread the love  MAHAKAMA ya Bermuda imetoa amri ya kufilisiwa kwa Kamapuni...

error: Content is protected !!