Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Michezo Kiongozi Simba amchukulia fomu Karia
MichezoTangulizi

Kiongozi Simba amchukulia fomu Karia

Spread the love

 

Aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba Swedy Nkwabi pamoja na Philemon Ntahilaija wamejitokeza kwenye makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kumchukulia fomu Wallace Karia kwenye uchaguzi Mkuu wa Tff utakaofanyika tarehe 7 Agosti, 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Uchaguzi huo mwaka huu utafanyika mkoani Tanga ambao wadau hao wawili walimchukulia fomu Karia ambaye anatetea kiti chake cha Urais mara baada ya muda wa awali wa miaka minne kumalizika.

Wadau hao walifika kwenye ofisi hizo za Tff majira ya saa 8 mchana huku wakiwa na risiti za malipo ya benki kama gharama za fomu ambapo ilikuwa shilingi 500,000.

Mara baada ya kuchukua fomu hiyo kwenye ofisi za Tff Nkwabi alifunguka sababu za wao kumchukulia fomu Karia ili kutetea kiti chake na kusema kuwa wanataka aendeleze yale mazuri aliyofanya katika kipindi cha miaka minne.

“Mimi nimekuja kuchukua fomu kwa niaba ya Rais Wallace Karia, kumuomba kwamba atetee nafasi yake ya urais, aendeleze mazuri alishowahi kuyafanya katika kipindi hiki kinachofuata.” Alisema Nkwabi

Aidha Nkwabi aliongezea kusema kuwa kwa kiasi kikubwa Karia amefanikiwa katika uongozi wake hasa kwenye timu ya Taifa (Taifa Stars), sola la wanawake pamoja na mpira wa ufukweni (Beach soccer)

“Kwa kiasi kikubwa amefanikiwa sana, na nyie ni mashahidi mmeona mpira wa wanawake ulipofikia, beach Soccer na timu yetu ya taifa imeshikili mashindano yote muhimu na kiasi imefanya vizuri.” Alinena Nkwabi

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

error: Content is protected !!