Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kingwangalla kumshitaki Mwigulu kwa Magufuli
Habari za SiasaTangulizi

Kingwangalla kumshitaki Mwigulu kwa Magufuli

Spread the love

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangwalla ametoa siku saba kwa jeshi la polisi kuwakamata vigogo ndani ya jeshi hilo waliopanga njama za kumuua mwanaharakati wa kupambana na ujangili Wayne Lotter raia wa Afrika Kusini la sivyo atalishitaki jeshi la polisi kwa Amiri mkuu wa Tanzania, Rais John Magufuli. Anaripoti Dany Tibason.

Amesema kuwa iwapo jeshi la polisi ambalo Waziri wake ni Mwigulu Nchemba, halitaweza kutoa majibu na kuchukua hatua ndani ya siku hizo saba itakuwa ni hatua nyingine ya kuchukua kwani waliofanya uharifu wanajulikana na taarifa zipo lakini hazifanyiwi kazi.

“Nitamweleza Rais Magufuli ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu, awa majangili wanajulikana na majina nimewapa jeshi la polisi lakini hakuna hatua zinazochukuliwa siwezi kulinyamazia hili kwa kuangalia vyeo vyao au ukubwa wao,” amesema Kigwangwala.

Kigwangwala amesema kuwa haiwezekani jeshi la polisi likaendelea kukaa kimya wakati sisi hata majina yao tunayafahamu lakini chombo chenye mamlaka hakioneshi jitihada zozote kwa kuwafuatilia watu hao wakati mipango ya kufanya ujangili inajulikana ilivyokuwa ikipangwa.

Amesema hata watu ambao wanaendelea kutoa ushirikiano juu ya kupambana na ujangili wamekuwa wakiishi kwa hofu hivyo ni lazima jeshi la polisi litoe majibu haraka ili kuondokana na hofu ambayo inaonekana kuwepo.

Mbali na kutoa siku saba kwa jeshi la polisi pia ametoa siku saba kwa makampuni matano ya Uwindaji ambayo yana vibali halali vya uwindaji lakini kampuni hizo zimekuwa zikijihusisha katika vitendo vya uwindaji halamu na kufanya ujangili kinyume na makubaliano.

Dk. Kigwangwalla alitoa tamko hilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Swagaswaga uliopo katika ofisi ya Maliasili na Utalii mkoani Dodoma.

Akiendelea kuzungumza na waandishi wa habari juu ya mafanikio aliyoyafanya kwa muda wa siku mia moja tangu kuteuliwa na Rais Magufuli kushika Wizara hiyo Dk. Kigwangwala amesema kuwa lengo kubwa ni kuhakikisha anapambana na ujangili.

Dk. Kigwangwalla amezitaja kampuni tano ambazo zinatakiwa kutumia siku saba tu kwa ajili ya kujieleza.

Amezitaja kampuni hizo kuwa ni BrleteSafaris Corporation LTD, Game Frontiers of Tanzania LTD, Mkwawa Hunting Safari(T) LTD, Tanzania Game Trackkers Safaris LTD na Wengert Windrose Safaris (T) LTD.

Amesema kuwa katika kipindi cha siku miamoja ameweza kufanikisha mambo kadhaa ya kupambana na majangili na kueleza kuwa watuhumiwa 74 wamekamatwa kwa makosa mbalimbali na hatua za kisheria.

Mbali na kukamatwa wa watuhumiwa 74 kwa makosa mbalimbali pia wapo washiriki 949 ambao kwa njia moja au nyingine wamekamatwa kama washiriki wa kusaidia kufamikisha mipango ya ujangili.

Amesema wizara imekuwa ikifanya kila jitihada za kuhakikisha inabadilisha mfumo na ifikapo Julai mosi mwaka huu malipo yote yatalipwa kwa njia ya kielektroniki.

Amesema kuwa katika hatua nyingine ya kupambana na ujangili ni pamoja na kuwepo kwa ndege ambazo hazina Rubani ambazo zitakuwa zikifanya kazi ya kupambana na ujangili katika maeneo mbalimbali ya uhifadhi.

Akizungumza juu ya utatuaji wa migogoro Dk. Kigwangalla amesema kuwa kwa sasa wamejitahidi kutatua migogoro ya muda mfupi hususani kwa watu ambao wapo karibu na uhifadhi kwa kuwashirikisha katika uwekaji wa mipaka ya kudumu na isiyo hamishika.

Katika hatua nyingine Dk. Kigwangwala ametoa siku 30 kwa wale wote waliovamia kiwanja chenye hati 4091 kilichopo njiro mkoani Arusha na kujenga nyumba zao za kudumu.

Amesema kiwanja icho kilivamiwa na baadhi ya mawaziri wakuu wa staafu bila kuwataja majina, pamoja na maofisa mbalimbali wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

“Kiwanja hicho kilikuwa ni mali ya taasisi ya serikali ambayo taasisi tanzu ya Utalii (Bodi ya Utalii Tanzania) kuna vymba za watumishi wa serikali lakini pia kuna watu ambao wamejigawia viwanja na kujenga nyumba za kudumu.

“Sasa natoa siku 30 kwa wale wote ambao walivamia kiwanja hicho na kujigawia viwanja kuhakikisha wanapeleka hati zao kwa kamishina wa Ardhi ili waweze kuona kama kuna uwezekano wa kuendelea kumiliki viwanja hivyo,” amesema Dk. Kigwangwala.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!