July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kingunge kuibomoa CCM Mara

Spread the love

MWANASIASA mkongwe Kingunge Ngombare -Mwiru, anarajiwa kufunga kampeni za Mgombea ubunge Jimbo la Musoma Mjini, Vicent Nyerere (Chadema), Oktoba 24 mwaka huu ikiwa ni siku moja kabla ya uchaguzi mkuu. Anaandika Moses Mseti, Musoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo na Vicent Nyerere wakati na waandishi wa habari ambako amesema katika hatua hizi za mwisho wamekusudia kuvunja ngome za CCM na kujiongezea nguvu ya ushindi wa kishindo siku ya jumapili.

Nyerere ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mara, amesema kutokana na mwanasiasa huyo kuwa na ushawishi mkubwa kwa wananchi ana imani ataweza kuwabadilisha baadhi ya wafuasi wa CCM na kuungana na gari la mabadiliko.

“Mzee Kingunge Oktoba 24 mwaka tutafunga nae kampeni zetu hapa Musoma, katika siku hizi za mwisho tutaweza kufanya mabadiliko makubwa sana,” amesema Nyerere.

Nyerere amesema kuwa kada huyo aliyejiengua CCM mwezi huu mwanzoni, atakisaidia Chadema kuvunja ngome zote za CCM Oktoba 24 mwaka huu siku moja kabla ya uchaguzi Mkuu.

Kingunge ambaye ni anamiliki kadi namba nane ya CCM ni miongoni mwa makada 20 wa Tanu na Afro Shirazi Part (ASP) waliounda mfumo ulioanzisha CCM.

Hata hivyo Nyerere amesema kutokana na chama chao kuwa na nguvu na mvuto kwa Wananchi wana uhakika wa kushinda majimbo yote ya mkoa wa Mara na Tanzania kwa ujumla.

error: Content is protected !!