February 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

King’ora cha hatari chazua taharuki Bungeni, wabunge wapagawa

Wabunge wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kutokea hali ya hatari ndani ya ukumbi

Spread the love

SHUGHULI za Bunge limelazimika kusimama kwa muda baada ya kutokea hali ya taharuki ndani ya ukumbi wa bunge, baada ya kulia king’ola kinachoashiria na hali ya hatari na kusababisha wabunge kutoka nje bila kufuata utaratibu. Anaripoti Danson Tibason, Dodoma … (endelea).

Hali hiyo imetokea majira ya saa 10.58 wakati wa kipindi cha maswali na majibu muda mfupi baada ya Naibu Spika Dk.Tulia Akson kuuliza swali la Nyongeza kwa Naibu Waziri Maji na Umwagiliaji Jumaa Awesso na alipoanza kujibu ghafla king’ola kinachoashiria hatari kuanza kulia na kusababisha wabunge kuanza kuiga kelele na kukimbia kutoka ukumbi wa bunge na kwenda nje.

Kutokana na hali hiyo wabunge walianza kupiga kelele kwa kusema kuwa hatari, hatari na bila kufuata utaratibu unaotakiwa na kusababisha Mwenyekiti wa Bunge, Najima Giga kutangaza kuhairisha shughuli za Bunge.

Bado haijaeleweka kuwa nini kilisababisha kulia kwa king’ola hicho kinachoashiria uwepo na hali ya hatari, lakini baada muda wavunge wamerudi bungeni kuendelea na kikao hicho.

Hii ni mara ya pili kutokea kwa hali ya sintofahamu ndani ya ukumbi wa Bunge kwani wiki mbili zilizopita kulitokea mtafuruku baada ya kuingia bundi ndani ya bunge jambo ambalo halijawahi kutokea tangu kujengwa kwa ukumbi huo.

Pamoja na kutokea kwa bundi ndani ya ukumbi Spika wa Bunge alisema kuwa Bundi wa Mchana hana shida ila bundi wa usiku ndiye mwenye kuleta tatizo.

Tazama video hapo chini kuona hali ilivyokuwa

error: Content is protected !!